Afisa Mtendaji Mkuu
wa kampuni ya Dun&Bradstreet Credit Bureau, Miguel Llenas akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kanzidata za mkopo kwa wakopaji na
wakopeshaji nchini. Mfumo huo umezinduliwa jijini Dar es Salaam kuwawezesha
wakopeshaji kuwa na taarifa sahihi za wakopaji.
1. Afisa Mtendaji Mkuu
wa Kampuni ya Dun&Bradstreet Credit Bureau, Miguel Llenas, akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kanzidata za mkopo kwa wakopaji na
wakopeshaji nchini. Mfumo huo umezinduliwa jijini Dar es Salaam kuwawezesha
wakopeshaji kuwa na taarifa sahihi za wakopaji.
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Fedha kutoka BOT, Jerry Sabi, akizungumza namna mfumo wa
kanzidata za mkopo kwa wakopaji na
wakopeshaji unavyosaidia kukuza sekta ya fedha na uchumi nchini.
Na Mwandishi Wetu
KATIKA kudhibiti
wakopaji wasumbufu, Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa kushirikiana na Dun &
Bradstreet Credit Bureau Tanzania Ltd. imezindua rasmi kanzidata itakayowezesha
upatikanaji wa taarifa za fedha kwa wakopaji kwa lengo la kuwatambua
wafanyabiashara wanaokopa na kushindwa kurejesha kwa wakati.
Akizungumza katika
uzinduzi wa mfumo huo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa kitengo cha usimamizi wa
fedha kutoka BOT, Jerry Sabi alisema mfumo huo ni mapinduzi mapya ya kuwaezesha
taasisi za fedha kutoa mikopo kwa wingi.
Alisema BoT imeshatoa
leseni kwa kampuni kampuni hiyo ili kuchakata taarifa za wakopaji kutoka kwenye
kanzidata ya Benki Kuu.
Aidha, Afisa Mkuu
Mtendaji wa Dun & Bradstreet Credit Bureau, Miguel Llenas alisema kuwa
mfumo huo utasaidia benki na taasisi zinazotoa mikopo kuwatambua wakopaji
wasumbufu na kupunguza mikopo chechefu.
Alisema mfumo huo pia
utaongeza uwajibikaji katika kukopesha na kukopa, pia utasaidia wakopeshaji na
wadai kusimamia vitabu vyao vya mkopo na kuhakikisha viwango vya riba hulingana
na maelezo husika ya mkopaji na kukuza bidhaa za mkopo katika soko la
wakopeshaji.
“Pia inapunguza muda wa kupata mkopo kulingana
na taarifa za mkopo zilizopo kwenye ripoti zake hivyo kukuwezesha kama dhamana
ya mkopo wako mpya na kukupatia mkataba bora na wenye kiwango stahiki cha riba.
"Inampa
mkopeshaji taarifa sahihi za mchakato wa utoaji wa mikopo; ujumbe na mwongozo
wa tathmini ya mkopaji, pia kuwezesha kasi ya utoaji mkopo na usimamizi wa
wateja husika.
"Pia mtoaji wa
huduma anaweza kuongeza kasi ya upatikanaji wa wateja, kuelekeza na kusimamia
mipaka ya mkopo yao na kuboresha utoaji wa huduma hizo.
Akifafanua zaidi kuhusu
huduma hizo, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Adebowale Atobatele alisema lengo lao
kila wakati limekuwa kutoa suluhisho la usimamizi kuelekea mikopo isiyolipika
katika sekta mbalimbali na kutoa taarifa sahihi kwa watoa mikopo kufanya
maamuzi sahihi ya kutoa au kutokutoa mikopo.
"Lakini pia
kuharakisha kasi yao ya kuchukua maamuzi; kurahisishaji upatikanaji wa haraka
wa bidhaa za mikopo kwa kampuni zinazostahiki, watu binafsi na hivyo kukuza
fursa za ukuaji kwa uchumi kwa wote.
“Pia tutaendelea
kufanya kazi kwa karibu na wadau wote na wahusika wote nchini ili kusaidia
kurahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi za mkopo nchini, "alisema.
Alisema kanzidata hiyo
itakuwa na taarifa za kihesabu ambazo wakopeshaji hutumia, pamoja na ripoti ya
mkopo kutathmini hatari ya kutoa mkopo.
"mfumo huu ni
njia muhimu za kukopesha ambayo inaweza kuamua ikiwa unapata mkopo, viwango
gani vya riba unalipa kwa deni husika, "alisema.
Naye Ofisa Mkuu wa
masuala ya Ufundi wa kampuni hiyo, Kelyn Pena alisema mfumo huo kwa watumiaji
wa kampuni hiyo wa kipekee nchini Tanzania kwa sababu inatoa taarifa halisi za
kitakwimu.
"Kanzidata hii ni
rahisi kutumiwa na taasisi za kifedha na watumiaji kwa jumla kwani iko thabiti
katika mpangilio wa wakati na utofauti wa historia ya mikopo ya watumiaji.
" alisema.
No comments:
Post a Comment