Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye akizungumza na
Mkuu wa Mkoa wa Sogwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela (hayupo pichani).
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye akisalimiana
na Mkuu wa Mkoa wa Sogwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela mapema leo wakati wa
ziara yake Mkoa wa Songwe.
Na Mwandishi Wetu
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye ameahidi kutoa
ushirikiano katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania
Dkt John Pombe Magufuli la kutoa ajira kwa vijana wazalendo waliopanda Mlima
Kilimanjaro.
Andengenye ametoa ahadi hiyo mapema leo kwa Mkuu wa
Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela alipofika ofisini kwake ikiwa ni
sehemu ya ziara yake Mkoani Songwe kukagua utendaji wa jeshi hilo Mkoani hapa.
“Suala la ajira
za vijana wazalendo waliopanda Mlima Kilimanjaro ili kumuenzi Baba wa Taifa
Hayati JK Nyerere kwa sasa linashughulikiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,
Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu na watakaponiletea majina niko tayari kutoa
ushirikiano.”, amesema Andengenye.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus
Mwangela amesema wakati wa kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru kilichofanyika
Mkoani Lindi Oktoba 14, 2019 Mhe Rais aliagiza Vijana wazalendo ambao walipanda
mlima Kilimanjaro na hawana ajira waangalie namna ya kuajiriwa.
“Tutashukuru sana endapo vijana wetu hawa wazalendo
watafanikiwa kupata Ajira, Nchi nzima walipanda vijana 84 kwetu Songwe tulitoa
vijana 21 kati yao vijana ambao hawana ajira ni vijana sita kutoka Songwe.”,
amesema Brig. Jen. Mwangela.
Wakati huo huo Andengenye amesema kuna mikakati ya
kitaifa ya kuboresha utendaji wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji na katika
Mikakati hiyo Mikoa mipya kama Songwe itapewa kipaumbele hasa katika kuongezewa
vifaa na watendaji.
No comments:
Post a Comment