Baadhi ya washiriki wa kikao kazi wakiwa wanafatilia mawasilisho wakati wa kikaokazi hicho.
Na Atley Kuni, OR-TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Doroth Gwajima, ameeapa kwamba
moto dhidi ya wabadhilifu wa dawa aliouwasha katika zoezi la ufatiliaji
hautazimika wala kupoa, huku akiwaomba wananchi kutoa ushirikiano wa karibu kwakuwafichua
watu/mtu yeyote atakaye bainika kuhujumu jitihada za serikali.
Gwajima ametoa kauli hiyo
ikiwa ni mara ya pili kurudia wito huo mbele ya Makatibu Tawala wa Mikoa,
wataalam Wafamasia kutoka mikoa 13 na wadau wa maendeleo Global Supply chain,
waliokutana mjini Dodoma kwenye ukumbi wa Mikutano wa OR-TAMISEMI katika kikao
kazi cha tathmini ya mbinu mpya ya kuimarisha takwimu za bidhaa za afya.
Akizungumza katika kikao
hicho Gwajima amesema, vita hiyo wataweza kuishinda kwa kuunganisha nguvu na
wananchi kutoka maeneo yote nchini.
“Niwaombe wanachi kuwa
mstari wa mbele kufichua wale wote mtakao wabaini wanahujumu suala la dawa
kwani vita hiyo siyo ya mtu mmoja mmoja wala serikali pekee bali niya jamii
nzima” alisema Gwajima na kuongeza kuwa, “wapo watu wanaotambua nani ni adui
wao katika vita hivi ndio maana jana nimeona kwenye Jamii forum wakinipa pole
na kunipongeza, lakini nasema lazima tutembee na wananchi katika hili.”
alisisitiza kiongozi huyo.
Gajima alisema inashangaza
unafika kwenye kituo ambacho kina wafamasia wasio pungua sita (6) lakini unakuta
kitabu cha kupokelea dawa (ledger) hakijahuishwa kwa zaidi ya miezi 5
hii ni hali ya hatari sana suala hilo halivumiki na wala hawezi kukubaliana nalo.
“Viongozi wangu Makatibu
Tawala, manaelewa tunatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2015-2020, hivyo
fatilieni hili hadi kwenye stoo za kutunzia dawa lakini pia ombeni taarifa na
ingieni kwenye mikutano yao muone kile wanacho kijadili maana humo hakuna zuiyo
lolote kwakuwa taarifa zinazo jadiliwa humo sio siri za mgonjwa, sasa wasije
wakajifichia kwenye mwamvuli wa taarifa za kitabibu kwakuwahadaa eti siri za
Mgonjwa hapana.” alikemea Gwajima.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mkuu wa Global Supply Chain Tukay Mavere alisema wachumi, watawala wa fedha
pamoja na watumiaji wa mfumo wa Supply chain kukaa pamoja na kuja na
mbinu mbadala za kudhibiti hali ya dawa na upatikanaji wake na kutoa mrejesho
wa kile ambacho serikali imewekeza.
“Lengo la mfumo huu
tunataka, tunachukua jambo, tunalichakata na kisha tunalitolea majibu kwa
wakati sio kungoja muda uende, aidha hii inakuwa ni zoezi endelevu katika
utendaji wa siku kwa siku kama mfumo ulivyo, hivyo tumeitana ili tuwe na
uwelewa wa pamoja juu ya hili tunalokusudia kulifanikisha” alisema Mavere.
Ka upande wao washiriki wa
warsha hiyo wamepongeza serikali na wadau kuja na mfumo huo, kwani nimatumaini
yao utakuwa suluhu ya yale wanayofanyia kazi kila siku.
“Kama Naibu Katibu Mkuu alivyosema,
mfumo huu utasaidia kuondoa ziada ya dawa unaosababisha upotevu wa pesa
kutokana na kuchina kwa Bidhaa zilizoingizwa bila takwimu sahihi vema sasa kila
mmoja wetu akitoka hapa awe mstari wa mbele katika kuutumia mfumo kwenye
utendaji wake.” alisema, Msalika Makungu
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Tabora.
Katika
kikao hicho cha siku
mbili pamoja na mambo mengine yatakayojitokeza, wataalam watajifunza
kupata
takwimu sahihi kwaajili yakufanyia maoteo kwakuwa mfumo unaanzia chini
kwenye huduma kwenda juu, hivyo itakuwa ni fursa ya kuwajengea
uwezo timu za uratibu wa afya za Mkoa na Wilaya, kupata taarifa sahihi
na
kufanya ugawaji dawa kulingana na mahitaji na kuondokana na tatizo la
dawa kwenye
maeneo yenye dawa nyingi. Mambo mengine ni kufanya bajeti kulingana na
rasilimali zilizopo lakini pia kuwezesha kufanya usimamizi kwa njia ya
mtandao
Online Supervision.
Katika kikao hicho, Wataalam
hao walikumbushwa juu ya viapo vyao kwa kuongozwa kiapo na Naibu Katibu Mkuu huku
wakiwa wamenyoosha mikono juu na kuapa kwamba, watakuwa chachu ya mapambano dhidi
ya ubadhilifu wa dawa na endapo wakishindwa basi wawe tayari kuachia nyadhifa
zao hata kwakutuma ujumbe wa maandishi kwenye mtandao wa kundi sogozi. (WhatsApp).
No comments:
Post a Comment