Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohammed Utaly, akizungumza na waandishi wa
habari ambao walitaka kujua mikakati ya wilaya yake kuhusu Uhifadhi na
Uendelezaji wa Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania
(TTCS). (Picha na Suleiman Msuya).
Na Suleiman Msuya
Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mohamed Utaly amesema serikali itachukua hatua kali za kisheria kwa kiongozi au raia ambaye atabainika kukwamisha mipango ya uhifadhi wa misitu inayotekelezwa wilayani hapo.
Utaly aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambao walitaka kujua mikakati wilaya katika kuendeleza Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS), unaotekelezwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (Mjumita) na Shirika la Kuendeleza Nishati Tanzania (TaTEDO) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo Uswis (SDC).
Alisema wilaya hiyo imekuwa na changamoto ya maeneo la kilimo lakini bado inahitaji kufanya uhifadhi wa misitu bila uvunjifu wa sheria.
Utaly alisema kwa sasa migogoro imepungua kwa asilimia 90 hivyo hatuvilia au kuhurumia mtu ambaye atatumia madaraka yake vibaya kuchochea vurugu.
Aidha alisema uhifadhi unaotekelezwa Mvomero unashirikisha wadau mbalinbali kama Mjumita, TFCG na wengine hivyo ni imani yake kuwa wasaidi wake watatumia mamlaka zao kuendeleza miradi hiyo muhimu kwa wiaya.
Mkuu huyo alisema pamoja na kupungua kwa migogoro hiyo bado kumekuwa na migogoro ya kushtukiza hasa ya wafugaji kuvamia misitu na kulisha mifugo yao na panapotokea kamati za ulinzi za misitu kukamata mifugo ndipo panapotokea mapigano na kuumizana akitolea mfano kijiji cha Kihondo na Maharaka kata ya Doma.
Alisema kwa muda mrefu masuala ya mapigano hayakuwepo hiyo ikichangiwa na ushirikiano uliopo baina ya Serikali za vijiji, wananchi, halmashauri na wadau wa mazingira na uhifadhi katika kulinda rasilimali misitu.
Utaly alisema wilaya inachokifanya ni kutawataka wakulima kuchukua alama za mifugo na kutoa taarifa kwa kamati ya ulinzi na baadae kufikishwa wilayani ili kuweza kuwadhibiti wafugaji ambao wamekuwa wakikimbia au kukana mifugo yao.
Pia alisema ushirikishwaji wa wananchi katika kila jambo ni muhimu na katika misitu kama halmashauri imekuwa ikiwafanya wananchi kushiriki katika uhifadhi wa misitu kwani wao ndio walinzi wa kwanza.
“Tunasisitiza utunzaji wa misitu katika maeneo yao kwani umeweza kuleta tija kwa kiasi kikubwa kwa misitu kutunzwa na wananchi kunufaika,"alisema.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwepo kwa mpango wa mkaa endelevu katika vijiji vyenye mradi kumeonyesha wananchi kufaidika na kukua kiuchumi tofauti na maeneo yasiyokuwa na miradi hiyo, hivyo wilaya imekubaliana kutenga bajeti yake ya mpango maalumu ili mradi utakapokamilika waweze kuendeleza wenyewe.
Alisema mradi wa mkaa endelevu umesaidia kupambana na migogoro ya wakulima na wafugaji baada ya kutengeneza mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo ya makazi, kilimo na ufugaji ambapo kama itatokea mmoja wao kuvamia atajulikana na kuchukuliwa hatua.
Aidha, alisema mradi huo umesaidia kuwaondoa vijana kwenye vitendo viovu kama wizi wa mifugo kwa kujitengenezea kipato kupitia mkaa endelevu na kushiriki katika shughuli za maendeleo huku halmashauri iki mapato kupitia fedha zinazopatikana kutokana na mkaa huo endelevu.
Ofisa Uraghibishaji wa Mjumita Elida Fundi alisema Mjumita na TFCG wamejikita katika uhifadhi wa misiti asili na wamelenga kuwafikia wananchi hasa wale wa vijiji na nia ni kusaidia jamii zinazoishi pembezoni mwa misitu ili ziweze kunufaika na rasilimali hivyo kwa kuitumia kwa ukaribu zaidi.
Fundi alisema mradi wa kuleta mageuzi katika sekta ya mkaa umekuwa ikitekelezwa katika vijiji 30 kwa wilaya tatu, na kwamba kumekuwa na kiwango kikubwa cha upotevu wa misitu ambapo zaidi ya laki nne ya misitu zimekuwa zikipotea kila mwaka na ardhi za vijiji ambazo hazina usimamizi kamilifu.
Fundi alitaja vijiji ambavyo vimenufaika na TTCS kuwa ni Maharaka, Msongozi, Misengele, Sewekipela, Kihondo, Ndole, Magunga, Diburuma, Masimba na Msolokelo
“Tumejipanga kusaidia vijiji kutenga matumizi bora ya ardhi, kutenga maeneo ya misitu kwa kutengeneza mipango ya kusimamia na kuweka sheria ndogo zitakazowasaidia,”alisema Elida.
Diwani wa kata ya Doma, Elimu Abdallah alisema mkaa endelevu umeweza kuwatoa wananchi wake kwenye umaskini, umeboresha utunzaji wa misitu na kutoa elimu ya misitu.
"Hapa kwangu mkaa endelevu ni fursa ya kipekee ya maendeleo ambayo tutaindeleza hata wafadhili wakiondoka," alisema.
Faustine Lucas Mkazi wa Kihondo, alisema mradi wa mkaa endelevu umeweza kubadilisha maisha yake na wanakijiji kiuchumi, maendeleo na mazingira.
Lucas alisema serikali inapaswa kuendeleza mradi huo hata kama wafadhili wataondoka.

No comments:
Post a Comment