Mjumbe wa Kamati ya Maliasili Tarafa ya Mazingara, wilayani Handeni
mkoani Tanga, Shabani Mtenguzi, akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu uhifadhi wa misitu wanaofanya kijijini hapo. (Picha Suleiman
Msuya).
Na Suleiman Msuya, Handeni
Na Suleiman Msuya, Handeni
MRATIBU wa Program
ya Kuendeleza Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Misitu (FORVAC) Kitaifa,
Emmanuel Msofe, amezitaka halmashauri na vijiji vyenye misitu kwenda
kujifunza uhifadhi na endelezaji misitu wilayani Handeni mkoani Tanga.
Msofe
alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao
walitembelea Msitu wa Tarawe uliopo katika Tarafa cha Mazingira wilayani
humo.
Alisema
Msitu wa Tarawe umejaliwa vivutio vingi huku ukiendelea kuwa msitu
asili kutokana wananchi kushirikiana na halmashauri kuutunza.
Msofe
alisema FORVAC imeamua kushirikiana na vijiji ili kuongeza mnyororo wa
thamani wa mazao ya misitu hali ambayo itaweza kuwanufaisha wananchi
kiuchumi, kijamii na maendeleo.
Alisema
FORVAC inatamani kuona halmashauri za wilaya na vijiji vyenye misitu
kutembelea na kujifunza namna ya kuendeleza rasilimali hiyo muhimu kwa
maendeleo ya nchi.
“Program
ya FORVAC inahakikisha rasilimali misitu inakuwa na mnyororo wa thamani
kwa kugusa jamii ambayo inazungukwa na misitu hiyo, hivyo nitumie
nafasi hii kuziomba halmashauri na vijiji vyenye rasilimali hiyo kuja
kujifunza hapa Handeni,” alisema.
Mratibu
huyo amezishauri halmashauri na vijiji kutumia fursa nyingine kama
vivutio vya utalii kuongeza mapato ya vijiji na halmashauri.
Msofe
alitolea mfano Msitu wa Tarawe ambao una vivutio vingi kama nyoka
wakubwa, pua mbili na eneo ambalo alipotea kungwi na mwali wake.
“Naomba
Mratibu wa FORVAC Handeni na ofisa maliasili kushirikiana na kijiji
kutangaza vivutio vilivyopo hapa Tarawe ni muhimu kwa maslahi ya wilaya
na vijiji,” alisema.
Mjumbe
wa Kamati ya Misitu Tarafa ya Mazingara, Shabani Mtenguzi alisema
mafanikio ya uhifadhi wa misitu saba iliyopo katika tarafa hiyo
yanatokana na kupatiwa elimu kuhusu faida ya rasilimali hiyo.
Alisema wananchi wamekuwa wakijitolea kuulinda misitu lakini bado kuna changamoto za vitendea kazi na majangili.
Mtenguzi
aliomba Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kutangaza
vivutio vilivyopo katika Msitu wa Tarawe ili watalii waweze kuja
kutembelea.
Katibu
Tawala (DAS), Wilaya ya Handeni Mwalimu Boniphace Maiga alisema
alipongeza Program ya FORVAC ambayo imekuja na malengo mengi ya kuongeza
thamani ya myororo wa mazao ya misitu na kuahidi kushirikiana nao.
Alisema
wilaya imeweka vipaumbele vyake ambapo moja wapo ni maliasili hivyo
watahakikisha taarifa sahihi zinawafikia wananchi kuhusu maliasili
zilizopo kwa kushirikiana na FORVAC.
Maiga
alisema wamefanikiwa kutambua maeneo ya vivutio vya utalii kama
mapango, misitu, mali kale na matukio kama ya Kibanga Kumpiga Mkoloni
ambapo watayatumia kutangaza wilaya yao.
No comments:
Post a Comment