Na Suleiman Msuya
TANZANIA
kupitia Shirika la Kimataifa linaloshughulika na masuala ya Haki za
Ardhi Landesa imepata fursa ya kuendesha Kampeni ya Haki Ardhi za
Wanawake duniani ambayo itadumu kwa miaka 12.
Kampeni hiyo ambayo imeanza 2018 inatarajiwa kutekelezwa hadi 2030 kwa vipindi vya miaka mitatu mitatu.
Hayo
yamesemwa na Mmoja wa Wakurugenzi wa Bodi ya Landesa Edna Sanga, wakati
akizungumza na waandishi wa habari ambao wameshiriki mafunzo ya siku
mbili mjini Morogoro.
Alisema
Tanzania imepata fursa ya kuzindua kampeni hiyo yenye kutaka wanawake
wanamiliki ardhi kutokana na mchango wao kwa jamii.
Sanga
alisema waandishi wa habari ni kiungo muhimu katika kutekeleza lengo
hilo la kimataifa lenye kutaka mwanamke anakuwa mmiliki wa ardhi kama
walivyo wanaume kwa kuandika habari ambazo zitachochea kundi hilo
kuonekana.
Alisema
kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa Novemba 21 mwaka huu na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na. Watoto Ummy Mwalimu.
"Landesa
imeamua kuwashirikisha waandishi wa habari ili wawe washiriki wa
kampeni hii, kwa miaka tisa tumekuwa tukizungumza umuhimu wa wanawake
kumiliki ardhi ili waweze kutumia waigeuze katika masuala ya kiuchumi
hivyo wakati ndio huu kwa kushirikiana katika kampeni hii ya kidunia,"
alisema.
Alisema utafiti
uliofanywa unaonesha ni asilimia 24 ya wanawake ndio wanamiliki ardhi
jambo ambalo linasikitisha kwani ulimwengu wa sasa unazungumzia uchumi
na uchumi unahitaji ardhi ili shughuli za kiuchumi, kibiadhara na
kijamii zinafanyika,"alisema.
Alisema
kampeni hiyo inapaswa kuwa ya kipekee ili iweze kuleta mabadiliko ya
kiungozi na ubunifu hivyo amewataka waandishi wawe wabunifu kuitangaza
kampeni hiyo muhimu ambayo imeanza kwa majaribio nchini.
Mkurugenzi
huyo alisema Tanzania imepata nafasi hiyo kutokana na utashi wa
kisiasa, sera, Sheria na ushirikiano uliopo katika kuinua mwanamke
kwenye umilili ardhi.
Sanga
alisema ujio wa kampeni hiyo ya Haki Ardhi za Mwanamke umechochewa na
kuwepo kwa sera na sheria ila utekelezaji ulikuwa duni hivyo kampeni
hiyo inayozinduliwa Novemba 21 itainua ari.
No comments:
Post a Comment