Baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo ya nadharia na vitendo kuhusu umuhimu wa kilimo hai kwa ustawi wa mtu mmoja mmoja na taifa. Mafunzo hayo yalifanyika Mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro, mwishoni mwa wiki.
Na Irene Mark, Moshi
WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia fursa za kilimo hai kisichotumia madawa na mbolea za kemikali kwa kuwa soko la mazao hayo ni kubwa duniani.
Ushauri huo ulitolewa mjini Moshi na Mshauri wa Mawasiliano kwenye Kilimo hai Tanzania, Constantine Akitanda wakati wa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili kufahamu kwa kina shughuli za kilimo hai, fursa, changamoto na faida zake kwa mkulima na taifa.
Alisema soko la Dunia la mazao yaliyolimwa kwa mbolea za asili ni kubwa na kwamba kuna uwekezaji wa Dola Bilioni 81 za Marekani linahitaji mazao hivyo ni wakati wa watanzania kutumia fursa hiyo.
"Watu wameamka sasa hivi wanataka kula vitu vya asili na bei yake ipo juu tofauti na hayo mazao yanayolimwa kwa mbolea na madawa yanayotengenezwa kwa kemikali," alisema Akitanda.
Alisema upo mkakati wa Bara la Afrika kuondokana na mazao yanayolimwa kwa kemikali miaka 50 ijayo kutoka sasa.
Kwa mujibu wa Akitanda, kilimo hai ni mkusanyiko wa maarifa ya zamani, akili na Sayansi katika kuandaa shamba na kutengeneza mbolea, mbegu na dawa za asili kwaajili ya kilimo.
Alisema faida za kilimo hai ni pamoja na kuondoa maradhi kwa binaadamu hasa yasiyo ambukiza na kumfanya aishi miaka mingi.
Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Tanzania Organic Agriculture Movement (TOAM), Richard Mhina alisema umefika wakati kwa watanzania kuacha matumizi ya mazao, vyakula na dawa zinazotengenezwa kwa kemikali kwa kuwa ni chanzo kikubwa cha maradhi yasiyoambukizwa.
"Najua changamoto zipo ila tunachotakiwa ni kuhakikisha elimu sahihi ya ubora wa kutumia vitu vilivyoandaliwa kwa njia ya asili inawafikia wananchi wote," alisema Mhina.

No comments:
Post a Comment