Na Irene Mark
WAFANYABIASHARA wadogo 'wamachinga' wa Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, wameishukuru Benki ya CRDB kwa kuwapa fursa rahisi ya mikopo ya Jiwezeshe.
Wamachinga hao ni wote wanaomiliki vitambulisho vya biashara vilivyotolewa na Rais John Magufuli.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jiwezeshe, Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Japhet Kandege aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa Benki ya kwanza nchini kuitikia wito wa Rais Magufuli wa kuwawezesha wamachinga ambao wengi ni vijana.
“Ni fahari sasa kuona vitambulisho vya Magufuli, vikizidi kuleta neema kwa wajasiriamali wetu wamachinga kupitia mikopo hii ya ‘Jiwezeshe’ kutoka Benki yetu ya CRDB.
"...Salamu hizi mlizotuletea Benki ya CRDB tutazifikisha kwa Rais Magufuli kumueleza namna ambavyo mmemuunga mkono,” alisema Naibu Waziri Kandege.
Nae Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk. Benard Kibesse alisema, "Benki ya CRDB mmeonesha njia kuwa hili linawezekana. Mwaka huu mmeanza na wajasiliamari 3,000 nawapa changamoto mwakani tukikutana kama hivi, muwe mmeshatoa mikopo kwa wajasiliamari 10,000 naamini mmnaweza," alisema Dk. Kibese.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema mikopo hiyo ya ‘Jiwezeshe’ inatolewa kidijitali kupitia huduma ya SimAccount ambapo wateja wataweza kukopa kuanzia kiasi cha Sh. 10,000 hadi Sh. 500,000 kupitia simu zao za mkononi.
“Mjasiriamali anatakiwa kufungua SimAccount kwa kupiga *150*62# kisha kujisajili kwa kutumia kitambulisho chake cha ujasiriamli, ambapo ataweza kunufaika na mkopo binafsi wa ‘Jiwezeshe’ au kupitia kikundi,” alisema Nsekela.
Kwa mujibu wa Nsekela wamezingatia mazingira ya biashara za wamachinga hivyo Benki ya CRDB haitatoza riba kwa asilimia, badala yake mteja atatozwa kati ya Sh. 500 na 1,000 wakati wa kurejesha mkopo.
“Tumefanya hivi ili kuwapunguzia mzigo wamachinga hawa ili wawekeze zaidi faidi wanayoipata kupitia mikopo hii ya ‘Jiwezeshe’,” alisisitiza Nsekela.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri aliwahamasisha wamachinga wa wilaya hiyo kuchangamkia fursa hiyo ya mikopo ya ‘Jiwezeshe’ kwa kujiunga na huduma ya SimAkaunti kwa ajili ya kinufaika na mikopo hiyo.

Baadhi ya wafanyabiashara wadogo wakiwa katika uzinduzi wa mikopo ya kuwawezesha wajasiriamali wa Wilaya ya Kigamboni.
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo wa Wilaya ya Kigamboni wakiwa katika uzinduzi wa mikopo ya kuwawezesha.
Mfanyabiashara akisoma taarifa zinazohusu Benki ya CRDB katika uzinduzi wa mikopo kwa wajasiriamali wa Wilaya ya Kigamboni.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wakiwa katika mkutano huo.
Wakinamama wakicheza kwa furaha wakati wa uzinduzi wa mikopo kwa wajasiriamali Wilaya ya Kigamboni.
NNaibu Waziri Ofis ya Rais TAMISEMI, Japhet Kandege, akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi
wa Mikopo ya kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wa Kigamboni.
Wajasiriamali wadogo wakitoa shuhuda za namna walivyonufaika na mkopo wa Benki ya CRDB.
Meza Kuu.
Mtoa mada, Prof. Limo.
Kikundi cha ngoma ccha Simba kikitumbuiza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mikopo kwa wajasiriamali wa Wilaya ya Kigamboni.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk. Benard Kibese, akitoa hotuba yake.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Japhet Kandege, akifurahia jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, DSara Msafiri.
Baadhi ya viongozi wa Benki ya CRDB pamoja na viongozi wa CCM, Serikali wakiwa katika uzinduzi huo.
Msanii Shilole akihamasisha wanawake kuchangamkia fursa za mikopo kutoka Benki ya CRDB.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, akitoa hotuba yake.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mikopo kwa wajasiriamali wa Wilaya ya Kigamboni, Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Japhet Kandege, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mikopo hiyo ambapo zaidi ya wajasiriamali 3000 wamenufaika.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mikopo kwa wajasiriamali wa Wilaya ya Kigamboni, Naibu
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Japhet Kandege, akizungumza wakati wa
uzinduzi wa mikopo hiyo ambapo zaidi ya wajasiriamali 3000 wamenufaika.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Japhet Kandege, akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela baada ya kutoa hotuba yake wakati wa
uzinduzi wa mikopo kwa wajasiriamali zaidi ya 3000.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Japhet Kandege, akipongezwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk. Benard Kibesse, baada ya kutoa hotuba yake wakati wa
uzinduzi wa mikopo kwa wajasiriamali zaidi ya 3000.
Baadhi ya wageni mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wafanyabiashara wadogo.
Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Japhet Kandege (katikati), akiwa ameshikana mikono na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela pamoja na viongozi wengine kama ishara ya uzinduzi wa mikopo hiyo.
Mgeni easmi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Benki ya CRDB pamoja na wadau wengine.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na watoa mada.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Wafanyakazi wa Ofisi ya mkuu wa wilaya ya kigamboni. wakiwa katika picha ya pamoja.
Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndigulie akimpongeza Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kwa kutoa mikopo kwa zaidi ya wajasiriamali 3000 Kigamboni. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri pamoja na Naibu waziri TAMISEMI, JAPHet Kandege.
Wajasiriamali wakiuza bidhaa zao wakati wa uzinduzi wa mikopo.
Wajasiriamali wakipata hudumba mbalimbali katika banda la Benki ya CRDB.
No comments:
Post a Comment