Ndugu wanahabari;
Napenda kuchukua fursa hii kwanza kuwajulisha kwamba Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini yamehamia rasmi Makao Makuu ya Nchi yaliyopo jijini Dodoma.
Pili, napenda kuwajulisha kuwa, hali ya nchi ni shwari kwani matukio makubwa yameendelea kudhibitiwa na yamepungua kwa asilimia 24.9%. Matukio ya Unyang’anyi wa kutumia silaha nayo yamepungua kwa asilimia 54.2% pia makosa
ya usalama barabarani yamepungua kwa asilimia 69.4%.
Aidha, Operesheni zinazoendelea katika Mikoa ya Kagera na Kigoma zinaendelea vizuri ambapo silaha mbalimbali za moto zikiwemo AK 47 pamoja na risasi zimekamatwa na baadhi ya watuhumiwa wameuawa katika mapambano na Jeshi la Polisi.
Pia waliohusishwa katika mauaji ya Watanzania wenzetu Mkoani Mtwara Operesheni za kuwasaka zinaendelea vizuri na baadhi ya watuhumiwa wameanza kukamatwa.
Ndugu wanahabari;
Kama mnavyofahamu kesho tarehe 24/11/2019 utafanyika uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Napenda kuwajulisha wananchi wote kuwa, Jeshi la Polisi limejiandaa ipasavyo kusimamia uchaguzi huo kuanzia kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo.
Wito wa Jeshi la Polisi kwa wananchi ni kwamba, kila mmoja afuate sheria, kanuni na taratibu kwani hakuna haki isiyokuwa na wajibu wa kutimiza. Kamwe asitokee
mtu wa kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani kwani atashughulikiwa kwa nguvu zote kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.
AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA
Imetolewa na:
David A. Misime - SACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania

No comments:
Post a Comment