HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 23, 2019

Mkutano wa 39 Baraza la Mawaziri wa EAC waanza jijini Arusha


Mwenyekiti wa Kikao cha Maafisa Waandamizi (katikati), Emmanuel Kamugisha , akizungumza na wajumbe (hawapo pichani) wakati wa kikao. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Fedha na Utawala, Mhandisi Stephen Mlote na kushoto ni Naibu Mkurugenzi Wizara ya Afrika Mashariki na Mahusiano ya Jamii wa Kenya, Raphael Kanothi.

Baadhi ya wajumbe kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Baraza la 39 la Mawaziri jijini Arusha.


Na Nelson Kessy, Arusha
 
Mkutano wa 39 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umeanza leo jijini Arusha kwa lengo la kujadili na kukubabaliana na agenda mbalimbali zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo (Summit) utakaofanyika mwezi Februari, 2020.
 
Mkutano huo wa siku saba umeanza leo kwa ngazi ya maofisa waandamizi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na utafuatiwa na mkutano wa Makatibu Wakuu kisha kuhitimishwa na Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo tarehe 27 na 28 Novemba, 2019.
 
Ajenda za mkutano huo zinakadiriwa kuwa tisa ambazo ni pamoja na ripoti ya utekelezaji wa maamuzi mbalimbali yaliyofikiwa na Baraza hilo kwenye vikao vilivyopita; taarifa kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, taarifa kuhusu masuala ya miundombinu, forodha na biashara; na ripoti ya kamati ya utawala na
fedha.
 
Agenda nyingine ni taarifa ya Baraza kwa Wakuu wa Nchi kuhusu utekelezaji wa maamuzi/maelekezo mbalimbali yaliyotolewa kwenye mikutano ya Wakuu wa Nchi; na
Kalenda ya Matukio ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha kuishia mwezi Juni
2019.
 
Jumuiya ya Afrika Mashariki inaundwa na nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini.

No comments:

Post a Comment

Pages