JOSE Mourinho |
LONDON, UINGEREZA
JOSE
Mourinho, ametangazwa rasmi kuwa kocha mpya wa Tottenham Hotspur ya London,
Uingereza, huku akifichua siri ya ‘kulamba matapishi yake’ na kukubali ajira ya
kuinoa Tootenham kuwa ni mipango sahihi waliyonayo.
Mourinho
aliyechukua mikoba iliyoachwa wazi na kocha aliyetupiwa virago juzi Jumanne, Mauricio
Pochettino, aliwahi kukaririwa mwaka 2015 akisema kuwa hawezi kamwe kuinoa
Spurs katika maisha yake, kwa sababu anawapenda mashabiki wa mahasimu wao
Chelsea.
Mourinho,
kocha wa zamani wa Chelsea na Manchester United, amesaini kandarasi ya kuinoa
Spurs hadi mwishoni mwa msimu 2022/23, huku akisema ubora wa Tottenham na kituo
chao cha soka la vijana ndio kitu pekee kilichomvutia kuingia mkataba huo.
"Ubora
wa vikosi vyote, ikiwa ni pamoja na timu ya vijana," alisema Mourinho juu
ya kilichombadili kauli yake ya kutoinoa Tottenham, na kuongeza: "Kufanya
kazi na wachezaji wa aina iliyopo Tottenham, ndicho kilichonivutia."
Mwenyekiti
wa Spurs, Daniel Levy alisema: "Katika Jose (Mourinho), maana yake nikuwa
tumepata kocha mwenye mafanikio na heshima kubwa katikaa mchezo wa soka."
Levy
amekubali kumlipa Mourinho mshahara wa pauni milioni 15 kwa mwaka, mara mbili
ya alivyokuwa akimlipa Pochettino na kibarua cha kwanza kwa kocha mpya kitakuwa
mechi ya London Derby dhidi ya mahasimu wao West Ham United, Novemba 23.
Chini
ya Pochettino, Tottenham ilifuzu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) msimu uliopita, lakini ikapoteza kwa mabao 2-0
mbele ya Majogoo wa Jiji Liverpool katika fainali kali mjini Madrid, Hispania.
Pochettino
raia wa Argentina, ambaye aliajiriwa Tottenham Mei 2014, hajawahi kuipa timu
hiyo taji lolote ikiwa chini yake, ambako ubingwa wao mwisho kwa Spurs ulikuwa
ni wa Kombe la Ligi mwaka 2008.
Levy
aaliongeza kuwa anaamini katika uzoefu alionao Mourinho na kwamba Mreno huyo
anaweza kuwa tiba ya anguko la klabu yake kwa kuamasha ari mpya katika vyumba
vya kuvalia vya timu hiyo, iliyohamia uwanja mkubwa zaidi mwaka huu.
Mourinho
ni kama yuko nyumbani jijini London, ambako anakumbukwa kwa kutwaa mataji
matatu ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) katika miaka ya 2005, 2006 na 2015,
pamoja na taji moja la FA aliyotwaa katika vipindi viwili vya kuinoa Chelsea.
Akiwa
na Manchester United kuanzia Mei 2016, Mourinho anayependa kujiita ‘The Special
One,’ alitwaa taji la Europa League na Carabao Cup 2017, kabla ya kutimuliwa
kazi klabuni Old Trafford Desemba 2018.
BBC
Sport
No comments:
Post a Comment