Meneja Mipango na Takwimu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Asteria Mushi, akizungumzia ongezeko la mapato kwenye Viwanja vya Ndege mbele ya waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne.
Na Asha Mwakyonde
SERIKALI kwa kushirikisna na mwekezaji binafisi inatarajia kujenga hoteli ya nyota nne kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, mwanzoni mwa mwaka 2020.
Ujenzi wa awali wa hoteli hiyo unatarajiwa kugharimu dola za marekani milioni 40.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Novemba 11, 2019, Meneja Mipango na Takwimu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Asteria Mushi, amesema kuwa mpango huo unatokana na mafanikio waliyopata katika kipindi cha miaka minne.
Sambamba na ujenzi wa hoteli hiyo wana mpango wa kujenga majengo mengine ya biashara yatakayokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Terminal III, lengo likiwa ni kuboresha huduma na kuwa chanzo cha mapato.
.
Amesema TAA wanatoa eneo lenye ukubwa wa square meter 25,000 lililopo Terminal II. “Kwa kuwa tunashirikisha sekta binafsi lazima tufuate sheria za Public and Private Partinership (PPP), ambayo ina haki zake za kuandaa mradi na imeshafika hatua ya tatu.

"Tenda itatangazwa kwa njia ya ushindani
atakayefanikiwa ndiye atakuwa mzabuni na tunatarajia hadi 2020/2021 atakuwa amesaini mkataba, kwa hiyo ujenzi unaweza kuanza mwanzoni mwa mwaka wa fedha 2022,” alisema.
Meneja huyo ameongeza kuwa katika kuboresha huduma zaidi, wanatenga asilimia 30 ya majengo ya abiria yawe kibiashara ambayo yatakuwa yakitoa huduma kwa abiria na wengine wanaotumia uwanja.
“Tunaangalia na ongezeko la abiria, na kubainisha kuwa ndege ya Air Tanzania ina njia karibu 10 za ndani na njia 5 za kimataifa.
“Hizo zimeleta chachu kwenye viwanja, kuna ndege zingine zimerudisha njia kama Air Zimbabwe na Uganda hayo ni mafanikio ya viwanja vya ndege,” ameeleza.
Amefafanua kuwa katika kipindi cha miaka minne iliyopita shughuli zilizofanyika ziliongeza mapato kutoka Sh. Bilioni 63 hadi Bilioni 105 kwa mwaka 2018.
Kwa mujibu wa Meneja huyo wa TAA, matarajio ya mamlaka yake ni kufikisha Sh. Bilioni 130 mwaka 2019/2020.
Amesema kwamba kuna ongezeko la asilimia 66 ya mapato ambapo bado Mamlaka hiyo inafanya shughuli zingine za kibiashara na kuongeza kuwa usafiri wa anga unakua na kuongeza pato la taifa na maeneo mengine.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Uhandisi na Huduma za Ufundi, Mhandisi Mbila Mdemu, alisema Serikali imetoa Sh. Bilioni 80 kwa ajili ya fidia kwa wananchi waliopisha upanuzi wa viwanja vya ndege nchini.
Amesema wameboresha viwanja mbalimbali vya ndege huku vingine vikifanyiwa upembuzi yakinifu kwa kujenga barabara za lami pamoja kupata hati miliki kwa baadhi ya viwanja vya ndege.

No comments:
Post a Comment