Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuwa utendaji kazi katika wilaya ya Mvomero umekuwa wa hovyo na
usiozingatia maadili jambo linalopelekea wilaya hiyo kuongoza katika mkoa wa
Morogoro kuwa na migogoro mingi ya ardhi sambamba na malalamiko mengi ya
wananchi dhidi ya ofisi ya ardhi.
‘’Baadhi
ya watumishi katika ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Mvomero mnajifanya ni
Maafisa ardhi au Wapima wakati hamkuajiriwa kwa nafasi hiyo, mnasaini nyaraka
za ardhi na kuwaumiza wananchi’’ alisema Lukuvi
Waziri
Lukuvi alitembelea ofisi ya Ardhi katika halmashauri ya Mvomero na kubaini
‘madudu’ katika ofisi hiyo ambapo alibaini baadhi ya majalada ya wananchi
waliomba kumilikishwa ardhi tangu mwaka 2012 katika halmashauri hiyo kushindwa
kupatiwa hati huku.
Hali
hiyo ilimfanya Waziri Lukuvi kumuagiza Kaimu Kamishana Msaidizi wa Ardhi Kanda
Maalum ya Morogoro Erick Makundi kuhakikisha wale wote walioomba hati na
kutumiza vigezo vya kupatiwa hati wanapatiwa kufikia mwezi ujao Desemba 2019.
Pia ameagiza kufuatiliwa majalada 300 ambayo wamiliki wake wamekamilisha
taratibu za kupatiwa hati lakini hawajapatiwa.
Sambamba
na hilo Lukuvi aliagiza wafanyakazi wa ofisi ya ardhi katika halmashauri hiyo
wanaojitolea kutosaini nyaraka zozote za ardhi kwa kuwa baadhi yao wamekuwa
wakishiriki kutoza tozo kwa gharama za juu za shilingi 50,000 wakati gharama
halisi ni 20,000.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mwl Mohamed Utaly alieleza kuwa wilaya yake ina
tatizo kubwa la migogoro ya ardhi pamoja na jitihada kubwa inayofanywa na ofisi
yake kukabiliana na tatizo hilo na kuongeza kuwa mingine inachochewa na
uhamasishaji unaowafanya wananchi kukata tamaa.
No comments:
Post a Comment