Mwandishi Mwandamizi wa
Gazeti la TanzaniaDaima Suleiman Msuya, akipokea cheti cha ushindi wa
shindano la tunzo ya Umahiri katika Uandishi wa Habari za Sayansi
Afrika, kutoka kwa Profesa Soukeye Dine kutoka Senegali. Kulia ni Mkurugenzi
Mkuu wa Africa Technology Policy Studies Network Dk. Nicholas Ozar na wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),
Dk. Amos Nungu. (Picha na Mpiga Wetu).
Na Mwandishi Wetu
WAANDISHI
wa habari saba kati ya 24 wa vyombo vya habari, akiwemo Suleiman Msuya wa
Gazeti la TanzaniaDaima, wameng’ara kwenye Shindano la Tuzo ya Umahiri katika
Uandishi wa Habari za Sayansi Tanzania.
Tuzo
hizo zilizoanza kutolewa mwaka 2017, zinalenga kuhamasisha waandishi wa habari
kuandika taarifa za sayansi na kuhabarisha umma juu ya matokeo makubwa ya
utafiti wa kisayansi.
Tuzo
hizo zinazoratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa
upande wa Tanzania na Jukwaa la Bioteknolojia za Kilimo Afrika (OFAB) zimetolewa Novemba 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia
tuzo hizo za mwaka 2019 Mratibu wa OFAB Tanzania Dk. Filbert Nyindodi alisema
mwaka huu kulikuwa na ushindani mkubwa na waandishi wengi walituma kazi zao.
Dk.
Nyindodi aliwataja washindi wengine kuwa ni Davidi Rwenyegira kutoka Kituo cha Redio
EA ambaye amekuwa mshindi wa jumla, Daniel Semberya Gazeti la Business Time na
Sifuni Mshana ITV ambao watawasilisha nchi katika shindano la OFAB likatalofanyika Novemba 21 mwaka huu jijini
Mombasa Kenya.
Wengine
ni Elias Msuya wa Mwananchi, Fatma Abdul wa Daily News, Benson Eustace na Msuya
ambaye ni mshindi katika eneo la mwandishi anayekuja kasi katika habari za
sayansi.
Alisema
kazi 72 kutoka kwa waandishi 24 ziliwasilishwa katika shindano hilo ambalo
linafanyika kila mwaka kwa ngazi ya taaifa na Afrika.
Mratibu
huyo alisema kwa mujibu wa majaji kazi zote zilikuwa na ubora ambao unakidhi
vigezo hali ambayo ilisababisha ushindani mkubwa hasa katika kumpata mshindi wa
jumla.
“Kwa
mujibu wa majaji washiriki wote walitimiza vigezo wamepata zaidi ya alama 65,
kupata daraja B+ sio kazi ndogo. Ni ushindi mkubwa.
Bahati
mbaya sheria za kombe la dunia hatua ya mtoano lazima mshindi apatikane hata
kama ni kwa kurusha shilingi,” alisema.
Alisema
kutokana na ushindani uliokuwepo anaona kila mshinriki ni mshindi kwa kuwa
halikuwa jambo rahisi kuwapata washindi wa kwanza.
Dk.
Nyindodi alisema matumaini yake ni kuona wawakilishi wa nchi katika shindano la
OFAB wanaibuka washindi na kurejesha ushindi nchini.
Tuzo
hizo zilitolewa na Mkurugenzi wa COSTECH, Dk, Amos Nungu na washiriki wengine
wa mkutano wa Baraza la Sayansi Afrika wanaomaliza mkutano wao leo.
Kwa
mwaka jana mshindi wa OFAB Afrika alikuwa Mwandishi Calvin Gwabara kutoka Kituo
cha Redio cha Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).
No comments:
Post a Comment