Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Hamisi Kigwangalla, akizungumza na Menejimenti ya TANAPA na Wakuu wa Kanda wa Shirika hilo jijiini Arusha. (Picha na WMU).
Na Aron Msigwa –
WMU, ARUSHA
Waziri wa Maliasili
na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa nchini
(TANAPA) lifanye maboresho ya miundombinu ya huduma za dharula na uokoaji ndani
ya hifadhi ya mlima Kilimanjaro ili kuogeza usalama wa watalii wanaokweda 2kupanda
mlima huo.
Pia, amelitaka
shirika hilo liedelee kuboresha miudombinu ya malazi katika hifadhi hiyo ili
iweze kuendana na mahitaji ya sasa ya wapanda mlima na kuangalia uwezekano wa
kutafuta wawekezaji watakaojenga hoteli za kisasa kwa lengo la kuvutia watalii
wengi zaidi.
Dkt.Kigwangalla
ametoa maagizo hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya TANAPA
na Wakuu wa Kanda wa Shirika hilo jijiini Arusha.
Amesema hatua hiyo
imekuja kufuatia changamoto mbalimbali alizokutana nazo wakati akipada mlima
Kilimanjaro Septemba, 28 mwaka huu, akiwa ameambatana na kundi la Wasanii na
wadau mbalimbali kutoka taasisi za umma na binafsi.
Dkt. Kigwangalla ameieleza
Menejimenti hiyo kuwa katika zoezi lake la kupanda mlima Kilimanjaro kuna
changamoto alizibaini zikiwemo za kukosekana kwa miudombinu ya kutosha ya
huduma za uokoaji na malazi ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka ili kuongeza
ufanisi na idadi ya watalii wanaopanda mlima huo.
Kufuatia hali hiyo ameiagiza
TANAPA ianze kuboresha huduma za dharula na uokoaji pia ijenge vituo vya
kutolea tiba na huduma ya kwanza mlimani vitakavyokuwa na wataalam wa kuhudumia
watalii wanaopata matatizo wakiwa mlimani pia kuboresha huduma za malazi katika
baadhi njia za mlima huo.
Dkt.Kigwangalla amesema
changamoto hizo zikitatuliwa kwa haraka zitauwezesha mlima huo kupata idadi
kubwa ya watalii kuliko ilivyo sasa na kuiogezea serikali mapato.
Kuhusu uboreshaji wa
huduma za uokoaji (Rescue services) kwa watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro ameiagiza
TANAPA ifanye utaratibu wa kuazisha huduma ya viberege maalum (Zip line)
vitakavyokua vinatumika kushusha wapada mlima watakaokua wakipata matatizo ya
kiafya kwa haraka hata wakati wa hali mbaya ya hewa.
“Suala la matumizi ya
“Zip line” mliongezee nguvu ya kulitekeleza, hii itakua njia rahisi ya uokoaji na
itawajengea ujasiri wapada mlima waelewe kwamba hata kama watapata shida yoyote
ya kiafya wakati wa kupanda mlima wanajua wana uhakika wa usalama wa maisha yao
hata pale ambapo hali ya hewa ni mbaya na helikopta haiwezi kutua mlimani”
Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.
Amesema uwepo wa huduma
hiyo ya kisasa ya kushusha watalii wanaopata chagamoto za kiafya itawezesha
watalii kupata huduma mlimani kupitia vituo vya kutolea huduma ya kwanza
vitakavyojegwa mlimani ambavyo vitakua na wataalam wenye mafumzo watakaokuwa na
jukumu la kutoa huduma muda wote.
Kuhusu uboreshaji wa
huduma ya malazi mlimani Dkt. Kigwangalla ameonesha kuridhishwa na hatua
zinazoendelea kuchukuliwa na TANAPA kuboresha miundombinu ya malazi mlimani na kuitaka
iangalie uwezekano wa kuhamasisha
wawekezaji wakubwa kwenye ujenzi wa hoteli za kisasa.
Amesema uwepo wa
hoteli hizo pamoja na mambo mengine utaongeza siku za watalii kukaa mlimani
akitoa mfano wa hoteli nzuri na za kisasa zilizojengwa katika milima ya Alaps ambazo
zinatembelewa na watu maarufu kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Kufuatia maagizo
hayo, Kamishna wa uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Dkt. Allan
Kijazi amesema kuwa TANAPA inaendelea kufanya maboresho kwenye maeneo ya kulala
wageni ili yaweze kwenda na wakati pia yawe na uwezo wa kupokea wageni wengi pia
kuishirikisha sekta binafsi katika utoaji wa huduma mlimani.
Amesema kazi ya
kuainisha maeneo kwa ajili ya ujenzi wa hoteli za kisasa inaendelea na kwa
kuanzia maeneo manne yamekwishaainishwa kwa ajili ya uwekezaji na kuongeza kuwa
baadhi ya wawekezaji wamekwishajitokeza na kuonesha nia ya kujenga hoteli za
kisasa katika mlima huo.
Kuhusu uboreshaji wa huduma
za ukoaji mlimani amesema kwa sasa kuna maeneo yana miundombinu ya barabara
zinazowezwsha magari ya kubebea wagonjwa kufika katika baadhi ya maeneo na
kutoa huduma ya uokoaji.
Pia amesema wamekua wakitumia helikopta kutoa
huduma za uokoaji licha ya huduma hiyo kushindwa kufanyika kazi wakati wa hali
mbaya ya hewa na hivyo kulazimika kutumia machela za matairi zinazoendeshwa na
watu kuhudumia watalii wanaopata matatizo ya kiafya.
Aidha, Dkt. Kijazi amesema
TANAPA inaendelea kufanya maboresho ya huduma za dharula na uokoaji na itawasilisha
kwake taarifa ya utekelezaji itakayoainisha mpango wa ujenzi wa njia za kisasa
zitakazotumia viberenge maalum vya uokoaji vitakavyokua vikipita kwenye waya
(Zip line) ili kazi ya ujenzi wa njia hizo ianze mara moja.
No comments:
Post a Comment