Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John
Kabudi akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi ya
ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya
Afrika (AfDB) Bwana Stephen Karangizi mazungumzo hayo yamefanyika katika
makao makuu ya Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Abidjan Nchini Ivory Coast.
Afisa
Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika
(ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bwana Stephen
Karangizi (kulia) akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) wakati wa majadiliano
kuhusu kuandaa mkakati maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo maalum na ya haraka ya
msaada wa kisheria kwa Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP)
anayefuatia baada ya Bw. Stephen Karangizi ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John
Kabudi(Mb) akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi ya ushauri
wa kishheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB) mara baada ya kumaliza majadiliano kuhusu kuandaa mkakati maalum
kwa ajili ya kutoa mafunzo maalum na ya haraka ya msaada wa kisheria kwa Ofisi
ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP)
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John
Kabudi(Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu na
Mkurugenzi wa Taasisi ya ushauri wa kishheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) mara baada ya kumaliza majadiliano kuhusu kuandaa mkakati
maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo maalum na ya haraka ya msaada wa kisheria kwa
Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP). Wa pili kutoka kushoto
ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila.
Na Mwandishi Wetu
Tanzania na Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF)
iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) zimekubaliana kuandaa
mkakati maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo maalum na ya haraka ya msaada wa
kisheria kwa Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP) hususani katika
kusimamia mashauri katika mahakama na mabaraza ya usuluhishi ya Tanzania na ya
Kimataifa katika maeneo ya madini, biashara na usuluhishi na makampuni ya
Kimataifa pamoja na mafuta na gesi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.
Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo mara baada ya majadiliano na Afisa
Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya ushauri wa kisheria ya Afrika
(ALSF) Bwana Stephen Karangizi mazungumzo yaliyofanyika katika makao makuu ya
Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Abidjan Nchini Ivory Coast.
Prof. Kabudi amesema kuwa lengo la majadiliano hayo ni kuisaidia
Tanzania kuweka mikakati kuimarisha sekta ya Sheria ikiwa ni pamoja na
kuiongezea uwezo ofisi ya mwanasheria mkuu wa Tanzania hasa baada ya mabadiliko
makubwa yaliyofanywa ya muundo mpya wa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali
ili kuiwezesha kutoa ushauri wa kina na wa kitaalam kwa serikali lakini pia
kusimamia mashauri katika mahakama na mabaraza ya usuluhishi ya Tanzania na ya
Kimataifa.
Ameongeza kuwa maombi ya Tanzania kwa taasisi hiyo kwa ajili ya
kuisaidia ofisi ya mwanasheria na wakili mkuu wa serikali yamekamilika na
kinachosubiriwa hivi sasa ni kuwasilisha maombi hayo kwa kikao cha bodi ili
utekelezaji uanze.
Ameongeza kuwa eneo jingine ambalo Tanzania inahitaji msaada
kutoka kwa Tanzania na Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika
(ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ni kuhusu kuisaidia
Tanzania katika hatua iliyoichukua ya kutunga sheria mpya ya usuluhishi wa
migogoro ya kimataifa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kuanzisha kituo kipya
cha kusimamia usuluhishi wa migogoro.
Katika eneo hilo Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF)
iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itatoa wataalamu kusaidia
Tanzania kupitia miswaada ambayo imeandaliwa na serikali pia kuandaa
andiko la namna kituo hicho kitawekwa Tanzania na kukidhi matakwa ya kimataifa.
Kwa uoande wake Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo
ya ushauri wa kisheria ya Afrika Bw Stephen Karangizi amesema wamepokea ombi
hilo na kwamba wanasubiri maamuzi ya kikao cha bodi ili kuweza kuanda program
maalum kwa ajili ya kuimarisha na kuendeleza ofisi ya mwanasheria mkuu wa
serikali.
Ameongeza kuwa nchi nyingi za Kiafrika zimeshindwa katika
usuluhishi wa migogoro hususani ya kibiashara,madini,mafuta na gesi na maeneo
mengine na kuongeza kuwa suala hilo linapaswa kuwekewa mkakati maalum na
kutekelezwa kwa haraka ili kuepuka makosa yaliyokwisha kufanywa katika siku
zilizopita.
Taasisi hiyo ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyo chini
ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ilianzishwa kutokana na ombi la Mawaziri
wa fedha kutoka Afrika kwa lengo la kuzisaidia Nchi za Afrika kujijengea uwezo
katika masuala ya kisheria hususani katika madini,mafuta na gesi
pamoja na madeni ili kuziwezesha nchi za Kiafrika kuwa na uwanda sawa wa
majadiliano katika ngazi za Kimataifa kuhusu masuala ya kisheria yanahusu
biashara na makampuni ya Kimataifa.
No comments:
Post a Comment