Na Tatu Mohamed
TAASISI
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Ilala inamshikilia
Mkazi wa Mbagala, Hussein Hassan (43) kwa tuhuma za utapeli kujifanya
Ofisa wa Takukuru.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Takukuru
Mkoa wa Ilala, Christopher Myava, alisema pia mtuhumiwa huyo ameghushi na
kujitengenezea kitambulisho namba PCCB 1565 chenye jina Hussein M.
Mhando na cheo cha Principal Investigator ili aonekane kama Ofisa wa
Takukuru na kufanya utapeli kinyume na sheria.
Alisema
baada ya kupokea taarifa toka kwa wananchi wazalendo, kuwa mtuhumiwa
huyo anatumia kitambulisho cha Takukuru katika kufanya utapeli.
"Disemba
12 tulimuwekea mtego maeneo ya Pachoto Mwananyamala, kwa bahati mbaya
alikimbia baada ya kuona watu asiowafahamu karibu na gari namba T 618
DMS ambalo siku hiyo alikuwa analitumia.
"Takukuru
ilifanikiwa kulishikilia gari hilo na Disemba 16 baada ya kuona gari
linashikiliwa mtuhumiwa alijisalimisha na kukiri kujifanya Ofisa wa
Takukuru mwenye cheo cha Principal Investigator na kutumia kitambulisho
hicho," alisema.
Aliongeza
kuwa mtuhumiwa huyo pia alikiri kuwa baada ya kuwakimbia maofisa wa
Takukuru siku ya mtego alikimbia na kitambulisho hicho cha kughushi na
kukichana ili kupoteza ushahidi.
Myava alisema kuwa uchunguzi utakapokamilika hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mtuhumiwa kwa mujibu wa sheria.
"Natoa
rai kwa wananchi kujihadhari na matapeli wa jinsi hii. Endapo
watabainika wahalifu wowote wa namna hii watoe taarifa Takukuru kupitia
namba 113 simu bure ambayo inapatikana saa 24 na siku 7 za wiki ili
hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wakati," alisema.
No comments:
Post a Comment