Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia), akiwa na Rais wa Taasisi ya Masuala ya Uchumi na Maendeleo ya Afrika nchini Japan (AFRECO), Tetsuro Yano.
Na Asha Mwakyonde
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), ina upungufu wa
madaktari bingwa wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu (Neurosurgeons), pamoja na wa usingizi.
Hayo aliyasema jijini Dar es Salaam leo wakati wa ziara yake na Rais wa Taasisi ya Masuala ya Uchumi na Maendeleo ya Afrika nchini Japan (AFRECO), Tetsuro Yano, Waziri Ummy alisema rais huyo alikuja nchini kwa ajili ya kufuatilia uhusiano kati ya Japan na Tanzania katika sekta ya afya.
Alisema kuwa taasisi ya MOI ina madaktari bingwa wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu saba na kwamba wanaohitajika ni 13 na wausingizi waliopo ni watano huku wanaohitajika ni 15 na nchi nzima hawafiki 30.
" Nimeomba kupitia kwao kutufundishia madaktari hawa pia tumeomba kushirikiana nao katika ujenzi wa miundombinu ikiwamo vyumba vya upasuaji. Hapa MOI tunahitaji vyumba 13 lakini vilivyopo ni tisa tu," alisema.
Waziri Ummy alisema kuwa rais Yano walikuwa Dodoma na watasaidia Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), kuanzisha kituo cha matibabu pamoja na kuanzisha kiwanda cha kutengeneza maji maji ya dawa.
" Nineona nije nao hapa MOI ili kuweza kuwasilisha maombi yetu ya kwao kwa ajili ya kuboresha matibabu ya kibingwa ya Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahami,",alisema Waziri Ummy.
Aliongeza kuwa alimleta katika taasisi hiyo rais huyo ili kuwaomba awajengee kituo cha huduma za utengemao kwani mtu anaweza kupata ajali na akafanyiwa upasuaji na kwamba viungo vyake vikawa havijarudi katika hali yake ya kawaida.
"Wenzetu wa Japan wameendelea katika masuala ya teknolojia, miundombinu na ujuzi. Nimeona tushirikiane nao katika masuala haya," alisema
Alisema maombi hayo yamekubali na kwamba Tanzania na Japan rasmi kushirikiana hususani katika kujenga uwezo wa huduma za kibingwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo ya MOI , Dk. Respicious Boniface, aliishukuru serikali ya awamu ya tano kuwekeza katika sekta ya afya.

No comments:
Post a Comment