Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Sima, akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji mkoani Morogoro. (Na Mpiga Picha Wetu).
NA LULU MUSSA, OMR
NAIBU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa
Sima, amesema Serikali imefanya mapitio ya Kanuni ya Tathmini ya Athari
kwa Mazingira ili kurahisha uwekezaji nchi.
Akizungumza
na Wafanyabiashara na Wawekezaji katika Mkutano wa Mashauriano baina
yao na Serikali katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani Morogoro,
Naibu Waziri Sima amesema gharama za kulipia vibali zimepungua na idadi
ya siku pia imepungua kutoka siku 145 mpaka siku 95 hivi sasa.
“Ndugu
zangu marekebisho haya yote yanayofanywa na Serikali, yanalenga
kurahisisha mchakato wa tathmini ya Athari kwa Mazingira na kurahisisha
uwekezaji hapa nchini, Mfano awali gharama kwa vituo vya mafuta zilikuwa
zaidi ya Milioni kumi na kwa sasa gharama hizi zimepungua hadi kufikia
Milioni Nne na nyingine Milioni mbili” Sima alisisitiza.
Katika
hatua nyingine Naibu Waziri Sima, amesema Ofisi yake inaandaa Kanuni za
Wataalamu Elekezi wa Mazingira ili kurahisisha uwekezaji kwa kuwa
miradi yote ni lazima ipate cheti kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira (NEMC). “Tangu tumefanya mapitio ya Kanuni zetu,
malalamiko kutoka kwa wawekezaji yamepungua kwa kiasi kikubwa sana” Sima
alisisitiza.
Hata hivyo Naibu Waziri Sima
amewakumbusha washiriki wa Kikao hicho kuwa Mabadiliko ya tabianchi ni
tatizo kubwa duniani, na kutoa rai kwa umma wa watanzania kupanda miti
kwa wingi kupunguza athari za mabadiliko ya Tabianchi.
Amewaagiza
wawekezaji hasa wenye Viwanda kuhakikisha wanaanzisha vitalu vya miche
katika maeneo yao na kusisitiza kuwa ukaguzi wa masuala ya Mazingira
katika maeneo yao utaanzia hapo.
Mkutano huu wa
Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashara na Wawekezaji umelenga
kusikiliza na kutatua changamoto zao umefanyika katika ukumbi wa Hoteli
ya Glonency mkoani Morogoro na kuendelea katika Mikoa ya Pwani na Dar
es Salaam. Jumla ya Mawaziri na Manaibu Waziri 13 wanashiriki Mkutano
huu.
No comments:
Post a Comment