HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 01, 2019

SIMIYU WAWA GUMZO ‘BQ JUNIOR TENNIS OPEN 2019’

 Timu ya Tenisi iliyoshiriki mashindano ya wazi ya BQ ‘BQ Junior Tennis Open 2019’ yaliyomalizika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. kutoka kushoto Dotto Ilanga, Rebecca Kurwa, Hellen Mtaka, Esther Stephano na kocha wao Micky Bunaya.
otto Ilanga (U-8), kutoka timu ya tenisi Simiyu akirudisha mpira kwa mpinzani wake wakati wa michuano ya BQ 'BQ Junior Tennis Open 2019' kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, jana. Dotto alishinda seti 2-0. (Picha na Tullo Chambo). 

Na Mwandishi Wetu

TIMU ya Tenisi kutoka Mkoa wa Simiyu ikishiriki kwa mara ya kwanza kwenye mashindano ya Wazi ya BQ ‘BQ Junior Tennis Open 2019’, imeacha gumzo kutokana na kuonyesha ushindani mkali kwa wazoefu.

Mashindano hayo yamekuwa yakizoeleka kushirikisha wachezaji kutoka Arusha, Morogoro na wenyeji Dar es Salaam, lakini mwaka huu Simiyu imejitosa kwa mara ya kwanza, jambo lililopongezwa na wadau wengi.

Mashindano hayo yalianza kurindima Jumamosi na kufikia tamati jana kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, ambako Simiyu iliwakilishwa na wachezaji wanne, Rebecca Kurwa, Esther Stephano, Dotto Ilunga na Hellen Mtaka.

Katika Kundi la wachezaji chini ya miaka 10 (U-10), Rebecca Kurwa aliibuka mshindi na kutwaa medali ya dhahabu, Hellen Mtaka naye akishinda dhahabu U-6, Esther Stephano U-8 akifika fainali na kupoteza kwa seti 2-0 mbele ya Nasma Jumanne wa Dar es Salaam, wakati Dotto Ilanga akitolewa nusu fainali.

Kwa matokeo hayo kati ya wachezaji wanne, watatu wamefanikiwa kuondoka na medali.

Akizungumza wakati wa mashindano hayo, Kocha wa timu hiyo, Micky Bunaya, alisema ameridhishwa na viwango vya wachezaji wake, kwani ana miezi mitatu tu tangu aanze kuwanoa.

“Mchezo huu ni mgeni kabisa Simiyu, hivyo kutokana na Mkuu wa Mkoa, Mheshimiwa Mtaka (Anthony), kutaka vijana waendelezwe ilibidi aje Dar es Salaam kunichukua niende kufundisha na sasa ni miezi mitatu, lakini vijana wanaonesha maendeleo mazuri,” alisema Kocha huyo.

No comments:

Post a Comment

Pages