Na Irene Mark
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa taarifa ya uwepo wa vimbunga pacha katika Bahari ya Hindi jambo litakaloathiri mifumo ya hali ya hewa.
Meneja wa Kituo Kikuu cha Utabiri kutoka TMA, Samuel Mbuya (pichani), alisema hayo jana usiku alipotia taarifa ya vimbunga hivyo na tahadhari ya hali ya hew kwa siku tano kuanzia Disemba4, 2019.
Alitaja athari zitakazojitokeza ni vipindi vifupi vya mvua kubwa kwenye baadhi ya maeneo ya mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.
Alisema mamlaka hiyo pia inatoa angalizo la mvua kwenye mikoa 14 ya Tanzania ambayo ni Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Tanga, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Rukwa, Unguja na Pemba.
Kwa mujibu wa Mbuya, vimbunga hivyo vitaathiri pia shughuli za usafirishaji baharini hivyo kuwataka watumiaji wa bahari kuchukua tahadhari.
Kuhusu tahadhari za mvua Meneja huyo alisema baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na Pwani kwa siku tatu mfululizo kuanzia Disemba 4 hadi 6 mwaka huu.
"Maeneo mengi ya nchi yatapata mvua kwa siku hizi tatu hivyo lazima wananchi wachukue hatua kwa kusafisha mitaro na kuondoa vitu vinavyozuia maji," alisema Mbuya.

No comments:
Post a Comment