HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 13, 2019

WADAU WA ZAO LA ALIZETI WAKUTANA SINGIDA

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka akizungumza na wadau wa zao la alizeti mkoani Singida.
 Wadau wa zao la Alizeti wakiwa katika mkutano huo.
 

Na Mwandishi Wetu

WADAU wa zao la Alizeti wa Mkoa wa Singida wametakiwa kupanga mikakati ya pamoja ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo ili kutosheleza mahitaji makubwa ya viwanda vya kusindika ambapo kwa sasa vnashindwa kuzalisha mafuta kwa mwaka mzima kutokana na kukosekana kwa malighafi.

Akizungumza mkoani Singida katika Mkutano na Wadau wa alizeti,Wasindikaji, wakulima wa alizeti pamoja na watendaji wa Serikali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka, alisema ni vema mkoa wadau hao wakawwka mikakati ili kuhakikisha tatizo hilo halitokei tena.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa wao kama wadau wa zao la alizeti wanafursa kubwa ya kupata masoko ndani na nje ya nchi kutokana na jupendwa kwa mafuta yatokanayo na zao hilo.

"Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli inasisitiza uchumi wa viwanda na Viwanda havitaendekea kama wadau mtashinda kuweka mikakati imara ya uzalishaji wenye tija ili kuepuka kukosa malighafi,"alisena Mkurugenzi huyo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akiwahutubia Wadau wa Alizeti wa Mkoa wa Singida wakati akifunga rasmi mkutano wa kupanga mikakati ya kuongeza uzalishaji wa alizeti kukidhi mahitaji ya viwanda vya kusindika alizeti kwa mwaka mzima.

Dk. Nchimbi ameelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya zilizopo Mkoani Singida wahakishe wanaondoa Tozo zinazosababisha kero kwa Wakulima, Wasindikaji na Wafanyabiashara ya alizeti.

Mkutano huo umeandaliwa na TANTRADE kwa ushirikiano na Uongozi wa Mkoa wa Singida pamoja na  Chama cha Wasindikaji wa Mafuta ya  Alizeti Singida ( SISUPA) na kushirikisha Wadau wapatao 110 kutoka Mkoa wa Singida.

No comments:

Post a Comment

Pages