Mkurugenzi wa Jk Cement Amit Kothari akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichana) kuhusu makubaliano yaliyofanyika ya kufanya kazi pamoja na Kampuni ya rangi ya Goldstar Paints.
Mkurugenzi wa Jk Cement Amit Kothari akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Goldstar K. Srinivasan mara baada ya kusaini makubaliano ya kibiashara na Kampuni ya rangi ya Goldstar Paints.
Na Janeth Jovin
WATANZANIA wameshauriwa kutumia bidhaa Bora ya rangi ya Jk Wall Putty ambayo inaweza kupendezesha kuta za nyumba pamoja na kupata rangi inayoweza kudumu kwa muda mrefu.
Ushauri huo umetolewa jijini Dar es Salaam Jana na Mkurugenzi mkuu wa Jk Cement Amint Kothari katika hafla ya kutangaza kuunganisha kampuni mbili za Jk white Cement (Afrika) ltd ambayo ni sehemu ya Kampuni ya Jk Cement ya India na Kampuni ya uzalishaji wa rangi ya Goldstar Paints ya Tanzania ili kuingiza sokoni bidhaa mpya ya Jk Wall Putty.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mkurugenzi huyo anasema ni muhimu watu wakatumia bidhaa zao hasa za rangi kwasababu zina ubora na zinaweza kustahimili kwa muda mrefu na kuleta muonekano ang'avu na nyororo kwenye kuta.
Pia anasema rangi hiyo ya Jk Wall Puttt inaondoa uihitaji wa kutumia gypsum plaster ambayo ni njia inayozoeleka hapa nchini na kwamba Kampuni ya Goldstar Paints ikiwa na mzalishaji wa bidhaa Bora sokoni ,itatoa nafasi kwa Jk Wall Putty kuingiza sokoni kwa haraka zaidi.
Kuhusu ushirikiano huo Mkurugenzi Kothari anasema "sisi Kama Jk White Cement ,siku zote tumekuwa na azma ya kuzalisha bidhaa zenye ubora na huduma nzuri kwa wateja Wetu ,ikiwa timefanikiwa kufika maeneo mengi ulimwengu kwa kuwa na nembo na mikakati imara ya kukuza Soko la bidhaa zetu"anasema Kothari
Nakuongeza kuwa Goldstar Paints ni mshirika muhimu kwenye Safari hii kwani tuna dhamira na shabaha zinazoendana katika kuleta bidhaa zenye ubora na tunaamini kwamba hii hatua muhimu katika.kuleta ubunifu na kuongeza uwezo wa kuwahudumia wateja.
"Tunajivunia kuwa hapa Tanzania na tunategemea kuleta huduma zinazokidhi mahitaji ya wateja sokoni,na kwakweli wameamua.kuna nchini ni katika kuunga juhudi za serikali lakini serikali imekuwa ikihamasisha wawekezaji kuja kuwekeza."alisisitiza Kothari
Kwaupande wake Mkurugenzi mtendaji wa Goldstar Paints K Srinivasan anasema Kampuni yao imekuwa mastari wa mbele kwenye Soko katika kuhakikisha kwamba inaleta bidhaa zenye viwago stahiki
No comments:
Post a Comment