HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 19, 2019

WAVUVI 8 WA TANZANIA WASHIKILIWA KATIKA GEREZA LA NAKASERO NCHINI UGANDA



Na Lydia Lugakila, Kagera
  
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luaga Mpina, amemwagiza Mkurugenzi wa Uvuvi nchini kufanya mazungumzo na mwenzake wa Uganda ili kuona namna ya kuwaachilia watanzania 8 walioshikiliwa nchini Uganda.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Kanali Denice Mwila, amesema  serikali haiwezi kukubali wananchi wake kukamatwa na kushikiliwa wakati wakijitafutia liziki hivyo lazima ichukue hatua za nataka.

Waziri Mpina ametumia nafasi hiyo kumuagiza Mkurugenzi huyo Emmanuel Bonai kuhakikisha anamaliza suala la watanzania hao wanaoshikiliwa katika gereza la Nakasero Kidplomasia la maofisa wa Uganda.

Akitoa taarifa kwa waziri Mpina Mkuu wa wilaya ya Misenyi Kanali Mwila amesema watanzania hao walikamatwa wakidaiwa kuwa wamefanya Uvuvi katika maadhi ya Uganda kinyume cha sheria.

Amesema hakuna kosa katika hilo kwa sababu wilaya ya Misenyi haina uwezo wa kufanya Doria ya kujihakikishia mpaka.

Tanzania kupitia kikosi chake cha majini kwa kushirikiana na wilaya ya Misenyi inakabiliwa na ukosefu wa boti za doria zenye uwezo mkubwa wakati waganda wanatumia boti za jeshi kufanya shughuli kama hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages