Waogeleaji wa Bluefins wakishangilia baada ya kutwaa
ubingwa wa mashindano ya Morogoro.
Na Mwandishi Wetu
Klabu ya Bluefins
ya Upanga jijini Dar es Salaam imeshinda ubingwa wa mashindano ya kuogelea ya
Morogoro baada ya kukusanya pointi 2,621
na kuzipiku klabu nyingine zilizoshiriki.
Mashindano hayo yalifanyika kwenye bwawa la kuogelea la
Shule ya Kimataifa ya Morogoro (MIS) yalishirikisha jumla ya waogeleaji 190
kutoka klabu nne nchini.
Bluefins ambayo inaundwa na wachezaji chipukizi, iliweza kuzipiku klabu tatu,
Taliss-IST, Dar Swim Club na wenyeji, Mis Piranhas.
Mashindano hayo yalikuwa magumu na waogeleaji wa kike
wa klabu hiyo waliweza kukusanya jumla ya pointi 1,224 wakati wavulana walikusanya pointi 1,397 na
kuibuka kidedea.
Muasisi na kocha mkuu wa timu hiyo, Rahim Alidina
alisema kuwa ushindi huo umetokana na ushirikiano baina yao na makocha, wazazi,
wadau na juhudi za waogeleaji kuiletea sifa klabu yao.
Alisema kuwa walikuwa wanasaka mafanikio hayo tokea
mwaka 2018 baada ya kushinda nafasi ya pili na mwaka jana walishinda pia nafasi
ya pili.
“Haikuwa kazi rahisi kutwaa ubingwa huu, mashindano
yalikuwa magumu sana, nawapongeza wote waliofanikisha ushindi huu na kuanza
mwaka 2020 vizuri,” alisema Alidina.
Waogeleaji wa kike walioleta sifa katika klabu hiyo ni Aliyana
Kachra, Zainab Moosajee, Maryam Ipilinga, Alexis Misabo, Aminaz Kachra, Lina
Goyayi, Muskan Gaikwad, Filbertha Demello, Niharika Mahapatra, Yumna Hassan na Natalia
Ladha.
Waogeleaji wa kiume walioleta sifa ni pamoja na Mohammadhussein Imran, Kaysan Kachra, Sahal
Harunani, Moiz Kaderbhai, Jay Govindji,Raihan Abdullatif, Hassan Harunani,
Idris Zavery, Isaac Mukani, Kabeer Lakhani, Salman Yasser, Gervas Sayi na Delbert Ipilinga.
Pia wamo, Zac Okumu, Adam Patwa, Qais Kanji, Kahil
Walli, Christian Fernandes, Avinav Mahapatra, Aaron Akwenda, Shuneal Bharwani,
Enrico Barretto, Burhanuddin Gulamhussein na Rayyan Khan.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na klabu ya Taliss-IST
iliyopata pointi 2,583 wakati Mis Piranhas walimaliza katika nafasi ya tatu
kwa kupata pointi 1,914 na Dar Swim Club (DSC) ilipata jumla ya pointi 1907 na kumaliza katika nafasi ya nne.
No comments:
Post a Comment