Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
amelitaka Shirika la Nyumba la Tiafa (NHC) kuongeza kasi ya ujenzi wa
Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa iliyopo Musoma mkoa wa Mara ili kukamilika kwa muda uliopangwa.
Hospitali
hiyo ya Kwangwa ni ya ghorofa tano yenye shemu tatu (Wing A, B na C) na
inarajiwa kuanza kutoa Huduma kwa baadhi ya sehemu kati kati ya mwezi
ujao
Dkt
Mabula alitoa kauli hiyo jana tarehe 25 Februari mjini Musoma mkoa wa
Mara wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo unaofanywa
na NHC akiwa katika ziara yake ya siku moja.
Alisema,
pamoja na NHC kufanya vizuri katika ujenzi wa jengo la hospitali hiyo
ukilinganisha na wakandarasi waliotangulia lakini inapaswa kuongeza kasi
ili likamilike katika muda uliopangwa na kuanza kutoa huduma.
Kwa
mujibu wa Mabula, Hospitali ya Kwangwa itakayojulikana kwa jina la Mwl
Nyerere Memorial Hospital ina historia ndefu kwa kuwa pamoja na
kuasisiwa na Rais wa Kwanza Mwalimu Julius Nyerere lakini utekelezaji
wake unakamilishwa na serikali ya awamu ya tano.
‘’Ni
vyema NHC mkaongeza bidii katika ujenzi wa hospitali hii ili ikamilike
kwa haraka kwa kuwa hospitali hii ina historia ndefu na Rais John Pombe
Magufuli ameamua ujenzi huu ukamilike kwa kutoa bilioni 15’’ alisema
Mabula.
Katika
kuhakikisha ujenzi wa hospitali hiyo unakamilika kwa wakati, Naibu
Waziri Mabula alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa NHC Dkt Maulid Banyani
kusimamia kwa karibu maendeleo ya ujenzi huo sambamba na kupatiwa ratiba
ya mpango wa ujenzi na maendeleo yake kila baada ya siku mbili kwa nia
ya kufuatilia kwa karibu.
Hata
hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Dkt Maulid Banyani
alimuahakikishia Naibu Waziri Mabula kuwa, ujenzi wa hospitali hiyo
sasa utakamilika kwa wakati baada ya changamoto kadhaa ikiwemo ya
Mshauri Mwelekezi kupatiwa ufumbuzi.
Kwa
Upande wake Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima mbali na kuisifu NHC kwa
kufanya mabadiliko makubwa ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa
hospitali ya Kwangwa alioueleza kuwa ilikwamwa kwa mara kadhaa.
‘’Toka
Shirika la Nyumba la Taifa lianze ujenzi wa hospitali hii mwezi Agosti
mwaka jana kuna mabadiliko makubwa ya kasi ya ujenzi na tunataka
mjenge kwa wakati na viwango na Machi mwaka huu Huduma ya Mama na Mtoto
ianze kutolewa ‘’ alisema Malima.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, hospitali hiyo itatoa huduma kwa
wananchi wa mikoa ya Kanda ya ziwa pamoja na nchi jirani sambamba na
kutumika kama sehemu ya utalii kutokana na mazingira ya hospitali.
Historia
ya Ujenzi wa Hospitali ya Kwangwa iliyopo Musoma mkoa wa Mara inaanzia
mwaka 1977 pale Rais wa kwanza wa Mwl Nyerere alipotoa wazo la kujengwa
kwake lakini ujenzi huo umekuwa ukikwama kwa nyakati tofauti hadi Rais
John Pombe Magufuli alipotoa Shilingi Bilioni 15 kwa lengo la
kukamilishwa mradi huo ambapo sasa unatarajiwa kukamilika mwaka huu.
No comments:
Post a Comment