Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge amekabidhiwa Ofisi rasmi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Faraji K. Mnyepe kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli tarehe 06 Februari, 2020. Kabla ya uteuzi huo Balozi Kanali Ibuge alikuwa Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocol). Aidha, Balozi Ibuge anachukua nafasi ya Dkt. Faraji K. Mnyepe ambaye alihamishwa wizara kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa. Dkt. Mnyepe amechukua nafasi ya Dkt. Frolence Turuka ambaye amestaafu.
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akipokea baadhi ya nyaraka za Ofisi kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Faraji K. Mnyepe. Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akimpa mkono aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Faraji Mnyepe mara baada ya makabidhiano rasmi ya ofisi.
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Ramadhani Mwinyi baada ya kumtembelea ofisini kwake leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas D. Ndumbaro (Mb) akiwa na Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A.
Ibuge alipomtembelea Ofisini kwake leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment