Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Dk. Leonard Akwilapo, akizungumza katika kikao kazi cha Mradi wa (TESP).
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo,
amewataka wakufunzi wa vyuo vya ualimu waliopata mafunzo kupitia mradi
wa kuendeleza elimu ya ualimu Nchini TESP kuhakikisha wanaleta matokeo
yaliyokusudiwa kitaaluma ili kuisaidia sekta ya elimu kupiga hatua.
Dkt.
Akwilapo amesema hayo jijini Arusha wakati anafungua mjadala wa kufanya
tathimini ya mradi huo unaotekelezwa kupitia ufadhili wa serikali ya
Canada ambaye amesema zaidi ya Shilingi bilioni 90 zimetengwa kufadhili
mafunzo, vifaa pamoja na ukarabati na ujenzi wa miundombinu ambayo
ikitumika vema itaongeza kiwango cha elimu Nchini.
Wadau
wa utekelezaji wa mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu Nchini wakikutana
jijini Arusha, kubwa hapa ni kufanya tathmini ya mradi huo na kujadili
changamoto ili zifanyiwe kazi kwa lengo la kuendelea kuboresha Sekta ya
elimu.
Mratibu
wa Mradi huo Ignas Chonya amesema mradi ni wa miaka Mitano ambapo
Wakufunzi wa vyuo vyote 35 vya serikali sambamba na halmashauri 20
zilizo katika mpango zimefikiwa tokea kuanza kwa mradi huo.
Akizungumzia
umuhimu wa mradi huo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Dkt. Leonard Akwilapo amesema umezingatia changamoto zinazoikabili
sekta hiyo, ambapo pia vyuo vipya vitajengwa.
Ambapo
pia akasisitiza umuhimu wa Wadau kuhakikisha wanatekeleza vema mradi
huo ili uweze kuleta tija iliyokusudiwa kwa kuwa mstari wa mbele katika
kupokea mafunzo na kuyafanyia kazi ili kutoa matokeo.
Kansela
Mkuu wa ushirikino na Maendeleo kutoka Serikali ya Canada, Gwen
Walmsley amesema katika mradi huo zimetengwa zaidi ya bilioni 90
kuhakikisha mazingira ya utoaji elimu nchini yanaboreka.
No comments:
Post a Comment