Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akizungumza wakati wa ushiriki wa
kifungua kinywa cha pamoja na wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na
Benki ya NMB uliofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kutoka kushoto kwake ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilala - Jumanne Shauri, Meneja wa
Kanda ya Dar es Salaam - Badru Iddi, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za
Serikali wa NMB - Vicky Bishubo na Katibu Tawala wa
Manispaa ya Ilala - Charagwa Selemani.
Wakipata kifungua kinywa.
Wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Mwandishi Wetu
Benki ya
NMB inayoongoza kwa faida kubwa nchini, imeahidi kutumia bidhaa na
huduma zake kuzisaidia serikali za mitaa kufikia malengo yake ya
maendeleo na kuchangia ukuaji wa uchumi.
Ikiwa
tayari imefikisha huduma za kibenki kwa zaidi ya asilimia 99 ya wilaya
zote nchini kupitia mtandao wa matawi 224, zaidi ya ATM 800 na NMB
Wakala,
inayoifanya NMB iweze kutoa huduma za kibenki kwa serikali za mitaa
ziweze kutekeleza na kusukuma mbele agenda ya maendeleo.
Ikiwa na
umiliki wa soko wa asilimia 22 kwenye utoaji wa mikopo na amana za
wateja kunaifanya NMB kuwa Benki inayoongoza nchini kwa kupata faida
kubwa.
Kwa
mfano, mwaka jana NMB ilipata faida ya shilingi bilioni 148.6, ikiwa ni
ongezeko la asilimia 52 ikilinganishwa na faida ya shilingi bilioni 97.7
iliyopatikana mwaka uliotangulia. Kwa upande
wa mikopo, NMB ilitoa shilingi trilioni 3.61, ikiwa ni ongezeko la
asilimia 12 ukilinganisha na shilingi trilioni 3.27 zilizokopeshwa Mwaka
2018.
Hayo
yalielezwa mwisho wa wiki katika hafla fupi iliyoongozwa na Mkuu wa
Wilaya ya Ilala - Sophia Mjema, ikiwakutanisha wafanyakazi wa manispaa
na
wafanyakazi wa Benki ya NMB.
Akiongea
katika hafla hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikali wa NMB -
Vicky Bishubo, amesema Benki ya NMB imejidhatiti kuendelea kufanya kazi
na serikali za mitaa katika kusukuma mbele miradi mbalimbali yenye
lengo la kuboresha Maisha ya watu.
“Tunafanya
kazi na Manispaa na Halmashauri mbalimbali katika maeneo ya ukusanyaji
mapato ya serikali, kutoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo wadogo na wa
kati, wafanyakazi wa serikali, na kupitia
sera ya Benki ya majukumu ya kijamii kwa kusaidia huduma za elimu, afya
na majanga mbalimbali,” alisema.
Kwa
mfano, Benki ya NMB mwaka jana ilitoa zaidi ya dhamana 500 kwa
wakandarasi wazawa ili kuwawezesha kugharimia miradi mbalimbali ya
ujenzi nchini.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bi. Mjema aliwataka wafanyakazi
wa manispaa na wananchi wote wa Wilaya hiyo kutumia fursa mbalimbali
zinazotolewa
na Benki ya NMB katika kuendeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi na
nyingine kama mikopo ya nyumba.
Naye
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam - Badru Idd alisema kwa miaka yote
Benki ya NMB imekuwa ikitumia rasilimali na juhudi zake kutoa huduma za
kibenki kuwafikia wale ambao bado hawajapata huduma za kibenki hasa
wale wa vijijini.
#NMBKaribuYako
No comments:
Post a Comment