Naibu Waziri wa Kilimo, Omar Mgumba, akizungumza na wakulima wa zao la Muhogo nchini.
Naibu Waziri wa Kilimo, Omar Mgumba (kushoto), akipata maelezo ya bidhaa kutoka kwa Mjasiriamali.
Na Asha Mwakyonde
NAIBU Waziri wa Kilimo, Omar Mgumba, amewataka wakulima wa zao la Muhogo nchini kufuata maelekezo ya wataalamu kwenye matumizi sahihi ya mbegu bora na safi badala ya kutumia mbegu yoyote bila kuzingatia hali ya ekolojia.
Pia Waziri Mgumba amesema ni vema wakulima wa zao hilo nchini wakalima kwa tija ili waweze kutosheleza masoko ya ndani na nje ya nchi.
Hayo ameyasema jijini Dar es Salaam Februari 8, mwaka huu wakati akizindua Umoja wa Wazalishaji na Wasindikaji wa Zao la Muhogo nchini (TACAPPA), katika mkutano wa wadau wa muhogo ulioandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).
Amesema kuwa pamoja na uzalishaji huo changamoto kubwa katika zao hilo ni uzalishaji mdogo na wenye tija na kwamba zao la muhogo huzalishwa katika mikoa mbalimbali nchini kutokana na uwezo wake wa kustahimili mazingira tofauti ya ekolojia.
"Mwaka 2018, muhogo ulikuwa zao la pili kwa uzalishaji yenye asili ya chakula hapa nchini baada ya zao la mahindi na ulichangia zaidi ya asilimia 17 ambapo mahindi ilikuwa asilimia 37 na mchele asilimia 13 katika uzalishaji wa mazao ya chakula," amesema.
Waziri huyo ameongeza kuwa mwaka 2017/2018 uzalishaji wa muhogo ulifikia wastani wa tani nane kwa hekta moja ambayo iko chini ukilinganisha na viwango vya nchi zingine zilipofikia kama Indonesia, Nigeria ambao wao wamefikia zaidi ya tani 21 hadi 30, na hiyo ndio changamoto kubwa inayopelekea kushindwa kushindana katika masoko ya Kimataifa.
“Tija ndogo hutokana na matumizi hafifu ya mbegu bora, kutokuzingatia kanuni za mbegu bora, magonjwa mbalimbali yanayokabili zao hilo hasa batobato na michirizi ya kahawia, ukosefu wa masoko ya uhakika, ubora duni wa bidhaa tunazozalisha ambazo zinashindwa kushindana na bidhaa zingine kwenye soko la Kimataifa, matumizi hafifu ya zana za kilimo katika mnyororo wa thamani na matumizi finyu ya bidhaa za muhogo nchini” amesema.
Ili kutatua changamoto hizo Serikali imeboresha Sheria ya vituo vya utafiti wa mazao mbalimbali, kwa sasa kuna vituo saba maalum ambavyo vinafanya tafiti kwa ajili ya zao la muhogo ili kuja na mbegu bora zenye uwezo wa kupambana na magonjwa, mabadiliko ya tabia nchi na zenye tija hadi sasa aina ya mbegu 21 zimezinduliwa kwa ajili ya zao la muhogo pekee.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Edwin Rutageruka. amewasihi wazalishaji wa bidhaa hiyo kujipanga kupitia umoja wao kwa kupenya katika masoko , kuweza kuwahudumia wawekezaji nchini na kuongeza thamani zao hilo.
Ameongeza kwa kusema kuwa TanTrade imesimamia uanzishwaji na usajili wa umoja wa Wazalishaji na Wachakataji wa Muhogo Tanzania baada ya maazimio ya mkutano uliofanyika tarehe 28 Januari, 2019 lengo ni kuwa na sauti ya pamoja katika kuendeleza zao hilo
Pia Mkuu wa Wilaya Handeni, Tanga Godwin Gondwe, amesema kuwa kwa Mkoa wa Tanga wamelichukua kama zao la kimkakati katika kukuza uchumi kupitia kila kaya katika mkoa huo na wameona mafanikio makubwa kupitia zao hilo

No comments:
Post a Comment