Na Tiganya Vincent
MKOA
wa Tabora umeelezea kutoridhishwa na utendaji kazi wa Mmiliki wa
Kiwanda cha Nyuzi Tabora (New Tabora Textile) na kutaka kichukuliwe na
Serikali na kutafutwa mwekezaji mwingine anayeweza kukiendesha kwa
faida kwa ajili ya manufaa ya wakazi wa Mkoa huo na Taifa.
Kauli hiyo imetolewa jana
na Katibu Tawala Msaidizi( Uchumi na Uwekezaji) Mkoa wa Tabora Raphael Nyanda wakati
akiwasilisha taarifa ya uwekezaji kwa Mkoa wa Tabora kwa Wajumbe wa
Kamati ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Tabora walipokuwa wakipokea
taarifa ya utekelezaji
wa ilani ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Alisema
kuwa Mwekezaji wa sasa ameshindwa kukifanya kiwanda hicho kwenda kisasa
na kwa kulingana na soko la wakati huo na ujao na hivyo kutokuwa na
faida kwa uchumi wa Mkoa na nchi.
Nyanda
aliongeza kuwa Mwekezaji huyo anakwenda kinyume na lengo la Kiwanda
hicho ambalo ilikuwa kununua pamba nyuzi kutoka vinu vya kuchambulia
pamba na kuzalisha nyuzi kwa ajili ya kulisha viwanda vya nguo hapa
nchini na nje ya nchi.
Alisema
kuwa tayari Mkoa umeshaandika barua Ofisi ya waziri Mkuu, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Viwanda na Msajiri
ukipendekeza Kiwanda kiwe huru na kupewa mwekezaji mwingine.
Nyanya
alisema Mwekezaji alipopewa Kiwanda hicho Viongozi mbalimbali wa ngazi
ya wilaya hadi Taifa akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alitembelea Kiwanda hicho mwaka 2018 na
kuagiza kifufuliwe na kuanza kazi mara moja lakini Mwekezaji ameshindwa
kutekeleza agizo hilo.
No comments:
Post a Comment