Wanafunzi na walimu
waliokuwa katika hafla ya kupongezwa kwa kufanya vizuri katika matokeo ya
kidato cha nne na cha pili mwaka 2019. Hafla hiyo imeandaliwa na Idara ya elimu
Sekondari.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya
Canosa Sister Irine Nakamanya, akipokea cheti cha pongezi kwa shule hiyo kufanya
vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne na pili.
Na Mwandishi Wetu
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni,imepongezwa kwa kufanya vizuri katika matokeo ya kidato Cha nne na cha pili kwa miaka minne mfululizo kwa mkoa wa Dar es Salaam.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni,imepongezwa kwa kufanya vizuri katika matokeo ya kidato Cha nne na cha pili kwa miaka minne mfululizo kwa mkoa wa Dar es Salaam.
Pongezi hizo zimetolewa na Afisa
Elimu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Hamis Lissu wakati wa hafla ya utoaji
tuzo kwa walimu na shule zilizofanya vizuri kwa matokeo hayo kitaifa na kimkoa kwa
mwaka 2019 /2020.
Lissu amesema kuwa Halmashauri hiyo
imekuwa ikifanya vizuri na kwa ufanisi mkubwa kwa kila eneo ikiwemo Elimu, Afya na mazingira, Michezo na maeneo
mengine na kusema kuwa mafanikio hayo yanatokana na kuwa na Mkurugenzi mwenye
juhudi za kufanya kazi inayoendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa
na Dk. John Pombe Magufuli.
Lissi amefafanua kuwa Mkoa wa Dar es Salaam unajumla ya Halmashauri
tano lakini Halmashauri ya Kinondoni inayo ongozwa na Mkurugenzi wake Aron
Kagurumjuli imekuwa ikifanya vizuri katika sekta ya elimu ambapo imeongoza kuwa
na matokeo mazuri kwa miaka minne
mfululizo katika mkoa huo.
" Kinondoni imekuwa ikifanya
vizuri sana kwenye mambo mengi, binafsi mnanikosha na utendaji wenu uliotukuka
,niwasihi nguvu hii mliyokuwa nayo muendelee nayo ili kuendelea kuwa na rekodi
nzuri kwa kuwa mfano bora kwa Halmashauri nyingine zilizopo katika mkoa
wetu" amesema Bwana Lissu.
Lakini pongezi hizi pia zimuendee
zaidi Mkurugenzi Kagurumjuli, Kinondoni mmepata Mkurugenzi bora, anafanya
vizuri sana kwenye Halmashauri yake,na uchapakazi huu ndio anaoutaka Mhe. Rais
wetu Dk. Magufuli, tukiwa na wachakazi kama hawa, hakika kwenye mkoa wetu
tutakuwa na matokeo makubwa zaidi kwenye kila eneo” ameongeza Bwana Lissu.
Kwa upande wake Afisa Elimu
Sekondari, wa Halmashauri hiyo, Bwana Leornad Msigwa amesema katika matokeo ya kidato cha nne Kinondoni
ilishika nafasi ya 39 kati ya Halmashauri 195 na hivyo kufanya kupanda nafasi
tatu kitaifa ukilinganisha na mwaka 2018 ambapo ilishika nafasi ya 42 na
kuendelea kuongoza kwa kishindo kwa miaka mine mfufulizo katika mkoa wa Dar es
Salaam.
Msigwa ameongeza kuwa tathmini ya matokeo
ya kidato cha nne ya mwaka 2019
inaonyesha kuwa ufaulu umeongezeka kwa silimia 0.59 ukilinganisha na mwaka 2018
ambapo ufaulu umekuwa kwa asilimia 81.21 ambapo mwaka 2019 ufaulu ulikuwa kwa asilimia 81.80.
Kwa upande wa matokeo ya kidato cha pili , Msigwa
ameeleza kuwa tathmini ya upimaji wa
matokeo ya kidato cha pili kwa mwaka 2019 , ufaulu ulikuwa kwa silimia 94.04 na
hivyo kufanya Halmashauri ya Kinondoni kushika nafasi ya 24 kitaifa kati ya
Halmashauri 184 na hivyo kupanda nafasi 10 kitaifa ukilinganisha na mwaka 2018.
Msigwa amefafanua kuwa, katika
matokeo hayo mwaka 2019 watahiniwa
walikuwa 9,340 ambapo waliofaulu mtihani huo kati ya daraja 1-1V walikuwa 8,783
sawa na asilimia 94.04.
Amefafanua kuwa kati yao waliopata
alama za ufaulu wa daraja la kwanza ni 1,682, daraja la piIi ni 1,216, daraja la tatu 1,556, daraja la nne 4,329 huku
jumla ya watahiniwa 557 walipata alama ya sifuri.
Katika hatua nyingine Msigwa amewaeleza
walimu wa shule za Sekondari waliokuwa katika hafla hiyo kuendelea kujituma
zaidi kwa kutumia mbinu mbalimbali za ufundishaji ili kuwezesha Halmashauri
hiyo kuendelea kufanya vizuri zaidi kitaifa na kimkoa.
No comments:
Post a Comment