Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.
Palamagamba John Kabudi (Mb) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Ethiopia Dkt Workneh Gebeyehu walipokutana kwa ajili ya mazungumzo Mjini
Addis Ababa,Ethiopia Kando ya Mkutano wa 33 wa Wakuu wa Nchi na
Serikali wa Umoja wa Afrika.
Na Mwandishi Wetu, Adis Ababa
Tanzania
imeishauri Nchi ya Ethiopia kuchukua hatua ya kuchunguza kiini cha raia
wake kuondoka nchini humo kinyume na utaratibu na kwa njia zisizo
halali jambo linalosababisha mrundikano wa wafungwa ambao wanakamatwa
katika nchi wanazopita kama wahamiaji haramu ikiwemo Tanzania.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba
John Kabudi ametoa ushauri huo Addis Ababa Ethiopia anakohudhuria
mkutano wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika na
kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia kando ya mkutano huo Dkt.
Workneh Gebeyehu na ili kuchukua hatua za kudhibiti idadi ya raia wake
wanaondoka nchini humo na kukamatwa katika mataifa mengine Tanzania
ikiwemo.
Prof.
Kabudi amesema Mpaka sasa takribani raia zaidi ya 1,300 wanashikiliwa
katika magereza mbalimbali nchini Tanzania huku idadi ya wanaoendelea
kukamatwa ikiongezeka jambo linalosababisha mrundikano wa wafungwa
katika magereza ya nchi hiyo.
Ameongeza
kuwa katika mazungumzo hayo Tanzania na Ethiopia zimekubaliana kuchukua
hatua za pamoja zitakazowezesha kurejeshwa wafungwa na wahamiaji haramu
wan chi hiyo wanaoshikliwa Tanzania kwa utaratibu utakaokubalika baada
ya majadiliano ya kina na kitaalamu.
Akizungumza
kupitia kwa msemaji Waziri wa mambo ya Nje wa Ethiopia Dkt. Workneh
Gebeyehu amekiri kuwepo kwa tatizo la vijana wan chi yake kuondoka
nchini humo kinyume cha utaratibu na kuitumia Tanzania kama mapito
wakielekea katika nchi za kusini mwa Afrika na Ulaya na kuongeza kuwa
serikali ya nchi hiyo itachukua hatua madhubuti kukabiliana na hali
hiyo.
Pia
ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano wake katika suala la wahamiaji
haramu kwa kutoa taarifa za mara kwa mara kuhusu raia wa Ethiopia
wanaoshikiliwa Tanzania na kwamba wana imani kuwa mazungumzo
yatakayofanyika yatasaidia kuwarejesha raia hao nchini Ethiopia kwa njia
ya pamoja watakayokubaliana.
Kando
na masuala hayo ya wahamiaji haramu pia Prof. Kabudi na Dkt. Workneh
wamezungumzia masuala mbalimbali ya mashirikiano baina ya Tanzania na
Ethiopia ikiwa ni pmaoja na mashirikiano katika masuala ya
anga,miundombinu na ubadilishanaji wa utaalamu kuhusu ujenzi wa mabwawa
ya umeme ili kuziwezesha nchi hizo kupiga hatua za kimaendeleo katika
nyanja ya Uchumi.
No comments:
Post a Comment