Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (kushoto), akimkaribisha Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias
Kwandikwa, mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya kukagua
athari za mvua katika miundombinu ya barabara na madaraja, mkoani Simiyu.
Mhandisi
Mshauri kutoka kampuni ya Doch anayesimamia ujenzi wa barabara ya Maswa -
Bariadi (km 49.7) kwa kiwango cha lami, Samson Lulseged, akitoa maelezo ya hatua
ya mradi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, wakati alipoukagua na
kuridhishwa na kasi ya ujenzi wake, mkoani Simiyu.
Meneja
wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Simiyu Mhandisi Albert Kent,
akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, kuhusu hatua
zilizofikiwa katika ujenzi wa barabara ya Maswa - Bariadi (km 49.7), kwa
kiwango cha lami, mkoani Simiyu.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa,
akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Simiyu
Mhandisi Albert Kent, kuhusu umuhimu wa kuzingatia ubora unaoendana na thamani
ya fedha zinazotolewa katika ujenzi wa barabara ya Maswa - Bariadi (km 49.7),
kwa kiwango cha lami, mkoani Simiyu.
Na Mwandishi Wetu
NAIBU
Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, ametoa wito kwa Watanzania wote
kutoa taarifa katika mamlaka za Serikali zinazohusika usimamizi wa
miundombinu ya madaraja au barabara ambazo zimeharibika kutokana na mvua
nyingi za mwaka huu.
Naibu
Waziri Kwandikwa ametoa wito huo mara baada ya kuwasili mkoani Simiyu
katika ziara yake ya kikazi ya kukagua athari zilizotokana na mvua kubwa
zilizonyesha katika kipindi cha mwisho wa mwaka na zile za mwanzo mwa
mwaka huu katika miundombinu ya barabara ambayo imekamilika na ile
inayoendelea kutekelezwa.
"Niwaombe
Watanzania wenzangu mjue kuwa Serikali yenu haipendi mpate shida mkiona
sehemu barabara au daraja lina changamoto toeni taarifa hizo katika
mamlaka husika na vitashughulikiwa haraka zaidi iwezekanavyo",
alisisitiza Naibu Waziri huyo.
Aidha,
Naibu Waziri Kwandikwa amekagua mradi wa ujenzi unaoendelea wa barabara
ya Maswa - Bariadi kilometa 49.7 kwa kiwango cha lami na kuridhishwa na
kasi ya ujenzi wa barabara hiyo ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 78.
Naibu
Waziri huyo alisema kuwa hatua hizi za maendeleo za mradi huu unatokana
na kodi za wananchi na kuwapongeza watanzania kwa kuendelea kuunga
mkono Serikali yao kwa kulipa kodi na hivyo kurahisisha maendeleo ya
mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
"Hii
barabara inagharamiwa na fedha za ndani hivyo niwahakikishie kuwa kodi
zenu ndio matunda ya miundombinu bora na imara, uboreshaji wa afya,
Elimu na mambo mengine mengi ya kimaendeleo", alifafanua Naibu Waziri
Kwandikwa.
Mapema akitoa
taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo, Meneja wa Wakala wa Barabara
(TANROADS), mkoa wa Simiyu Mhandisi Albert Kent, alieleza kuwa mradi
huo mpaka sasa jumla ya kilometa 17.3 zimekamilika kujengwa kwa kiwango
cha lami na magari yameruhusiwa kupita ili kuepusha usumbufu hasa
vipindi hivi vya mvua.
Mhandisi
Kent amemuhakikishia Naibu Waziri kuusimamia mradi huo ambao unatakiwa
ukamilike mwezi Septemba mwaka huu kwa kuzingatia ubora unaoendana na
thamani ya fedha zilizotolewa.
"Mkandarasi
anaendelea vizuri na kazi ya ujenzi yakiwemo madaraja makubwa mawili
(Daraja la Simiyu na Banhya) na mengine madogo madogo pamoja na ujenzi
wa tuta la barabara katika maeneo mbalimbali," alisema Mhandisi Kent.
Naibu
Waziri Kwandikwa yupo katika ziara ya siku moja katika mkoa wa Simiyu
unaohudumia mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 923.65 ambapo
kilometa 334.33 ni barabara kuu, kilometa 521.62 barabara za mkoa na
kilometa 67.7 ni za barabara ya Wilaya ya Nkoma - Makao iliyokasimiwa.
No comments:
Post a Comment