HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 18, 2020

Mwakalinga ataka vijana, watumishi wajifunze ufundi stadi

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga, akizungumza na wanafunzi pamoja na watumishi wa Chuo cha Ujenzi Morogoro, alipofika chuoni hapo kukabidhi vifaa vya kufundishia wanafunzi ikiwemo mtambo mmoja (Grader) na Kompyuta 20.
 Mkuu wa Chuo cha Ujenzi Morogoro, Melkizedeck Mlyapatali, akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa Chuo hicho kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga (kushoto), alipofika chuoni hapo kukabidhi vifaa vya kufundishia wanafunzi ikiwemo mtambo mmoja (Grader) na Kompyuta 20.
 Wanafunzi wa Chuo cha Ujenzi Morogoro wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga (hayupo pichani), wakati akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa vya kufundishia wanafunzi hao ikiwemo mtambo mmoja (Grader) na Kompyuta 20, chuoni hapo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga (wa kwaza kulia) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa kukabidhi vifaa vya kufundishia wanafunzi wa Chuo cha Ujenzi Morogoro. Vifaa hivyo ni mtambo mmoja (Grader) na kompyuta 20.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga, akionesha Kompyuta alizozikabidhi kwa uongozi wa Chuo cha Ujenzi Morogoro, kwa ajili ya kufundishia wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho. Katibu Mkuu alikabidhi Kompyuta 20 na mtambo mmoja (Grader).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga, akitoka kukagua mtambo wa kufundishia (Grader), aliyoikabidhi kwa Uongozi wa Chuo cha Ujenzi Morogoro. (PICHA NA WUUM).

 
NA MWANDISHI WETU, MOROGORO

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Msanifu Majengo na Majenzi Elius Mwakalinga, amewataka wazazi, walezi, wafadhili na waajiri kuwapeleka vijana wao kupata mafunzo ya ufundi stadi ili kujiajiri.

Mwakalinga aliyasema hayo jana wakati akikabidhi mtambo aina ya (Grader) na Kompyuta 20 kwa Uongozi wa Chuo cha
Ujenzi Morogoro mkoani humo.
 
Katibu Mkuu huyo alisema kuwa hafurahishwi na kuwepo kwa idadi ndogo ya wanawake katika baadhi ya kozi, chuoni hapo hivyo ni jukumu la wazazi, walezi na makundi mengine kuwapeleka chuoni hapo.

"Nimesikitika kupata taarifa kutoka kwa mkuu wa chuo kuwa kozi nyingi zina idadi kubwa ya wanaume kuliko wanawake na nyingine zina wanaume pekee, elimu ya ufundi stadi ni kwa wote, shime jinsia zote kushiriki kupata mafunzo haya," alisema Mwakalinga.

Katibu Mkuu Mwakalinga, alifafanua kuwa utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana utatoa mchango mkubwa katika azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk. John Magufuli ya kujenga uchumi wa kati na wa viwanda ambapo fani za ujenzi ni muhimu katika kufikia azma hiyo.

Aidha, Mwakalinga aliupongeza Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kwa kukubali kutoa mtambo mmoja (Grader) na Wizara kutoa kompyuta 20 ili vitumike kufundishia wanafunzi.

Mwakalinga alisema vifaa hivyo vitakuwa chachu ya utoaji mafunzo chuoni hapo.

"Naamini sasa kuja kwa vifaa hivi kutarahisisha na kuhamasisha mafunzo kwa vitendo, nawasihi mtumie vifaa hivi kwa malengo yaliyowekwa pamoja na kuvitunza vizuri", alisisitiza Katibu Mkuu Mwakalinga.

Sambamba na hilo Katibu Mkuu Mwakalinga alisema kuwa Wizara ipo katika hatua za mwisho za kuanzisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi kwa kuunganisha Chuo cha Ujenzi Morogoro na Chuo cha Teknolojia Stahiki ya Nguvukazi kilichopo Mbeya.

Alisema lengo la kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kuboresha mafunzo yanayotolewa na vyuo hivyo viwili.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Morogoro, Melkizedeck Mlyapatali alisema chuo kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa watumishi wakiwemo wahandisi wa fani mbalimbali, wakufunzi, wahasibu na wafanyakazi wengine kutokana na wafanyakazi wengi kustaafu kwa mujibu wa sheria na wengine kufariki dunia.

"Chuo kina jumla ya wanafunzi 403 na kinaendesha mafunzo ya ufundi stadi na masomo ya kawaida kwa lengo la kuwezesha wahitimu kuwa mahiri katika Nyanja za ujenzi," alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages