Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) ,Josephati Kandege wa Pili kushoto akifanya Ukaguzi wa miradi
ya katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa, Mkoani Mwanza.
Na Geofrey Kazaula – BUCHOSA
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI
Mhe, Josephat Kandege ameuelekeza Wakala wa Barabara za Vijijini na
Mijini TARURA kuboresha Barabara katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa
Mkoani Mwanza ikiwa ni pamoja na kukarabati barabara zilizoharibiwa na
mvua.
Hayo
yamejiri wakati wa kukamilisha ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali
ya maendeleo katika Mkoa wa Mwanza ikiwa ni pamoja na kukagua hali ya
barabara zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini
TARURA.
“Kuna
maelekezo kwa TARURA kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI kuwa kwa fedha za
matengenezo ya barabara katika mipango yao, wahakikishe kuwa
matengenezo hayo yafanyike kwa kuaza na maeneo yaliyoharibika sana ili
kurudisha huduma kwa wananchi,’’ Amesema kiongozi huyo.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe, Charles Tizeba ameeleza kuwa
Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa ni mpya na hivyo haina Barabara za lami
na kuomba Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA kujenga walau
kilomita chache kwa kiwango cha lami ili Halmashauri hiyo iweze
kupendeza.
‘‘Halmashauri
yetu ni mpya na haina barabara za lami hivyo kwakweli naomba TARURA
waone namna ya kutusaidia ili Buchosa nayo ifanane na Halmashauri
nyingine,’’ Amesema Mbunge huyo.
Naye
Mkurugenzi anaye simamia Barabara za Vijijini kutoka Wakala wa Barabara
za Vijijini na Mijini TARURA Mhandisi Abdul Digaga amefafanua kuwa
tayari bajeti imetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara za lami
kwa Halmashauri ya Buchosa lakini pia matengenezo ya Barabara tayari
maelekezo yametolewa kwa nchi nzima kuhakikisha kipaumbele kina kuwa kwa
maeneo yaliyo haribiwa zaidi ili kurejesha huduma kwa wananchi.
“Tayari
maelekezo yametolewa kwa nchi nzima kuhakikisha matengenezo ya barabara
yanazingatia kipaumbele kwa kuanza na maeneo yaliyoharibika sana na
tunafanya hivi ili kurejesha huduma kwa wananchi wetu kwani yapo maeneo
yaliyoathiriwa na mvua kwa kiasi kikubwa,’’ Amesema Mhandisi Digaga.
Naibu
Waziri Kandege pia amesisitiza kuwa atafanya ufuatiliaji wa karibu na
kuhakikisha Hospitali ya Wilaya ya Buchosa inafunguliwa na kuanza kutoa
huduma kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya miradi aliyoitembelea.
No comments:
Post a Comment