Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Uchapaji wa Serikali Zanzibar, Khalfan Sheikh Saleh, wakati
akimueleza namna Wakala unavyotekeleza majukuu yake wakati alipotembelea Wakala
huo, Maruhubi, Zanzibar.
Na OWM, ZANZIBAR
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko ameeleza kuwa Katika
kuhakikisha kuwa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali inakidhi mahitaji ya
wateja wake kwa kuzingatia ubora wa huduma, ameitaka idara hiyo kuwekeza kwenye
matumizi ya mashine za kidigitali ambazo
zina uwezo wa uchapaji kwa kasi kubwa, viwango bora na kwa idadi kubwa ndani
ya muda mfupi.
Akiongea mara baada kutembelea
Wakala wa Uchapaji wa Serikali Zanzibar kwa lengo la kujionea namna Wakala
inavyotekeleza majukumu yake, Katibu Mkuu Mwaluko amefafanua kuwa amevutiwa na
utekelezaji wa majukumu ya Wakala kwa kuwa inaendesha shughuli za uchapaji
kibiashara, inao usimamizi mzuri wa ubora unaozingatia teknolojia ya kisasa ya
uchapaji, hivyo Idara ya Mpiga chapa Mkuu wa serikali ya Tanzania bara, hainabudi kutekeleza majukumu yake kama
ilivyo kwa Wakala.
Kwa upande wake Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Uchapaji wa Serikali Zanzibar, Khalfani Sheikh Saleh, amefafanua
kuwa Wakala umewekeza kwenye mashine za kidigitali na wamewajengea uwezo
wafanyakazi wake, ambapo kutokana na uwezo huo wamefanikiwa kukidhi mahitaji ya
wateja wake kwa wakati na kwa ubora husika.
Aidha, Mkurugenzi huyo
ameeleza kuwa Wakala wamefanikiwa kutekeleza Mpango wao wa biashara kwa kupata soko
la uhakika la uchapaji hususani kwa Taasisi na idara za serikali pamoja na
sekta binafsi, hivyo wamefanikiwa kuongeza mapato ya Serikali kupitia fedha zinazopatikana
kupitia kazi za uchapaji na ununuzi wa vifaa vya ofisi na kuandikia.
Tangu mwaka 2018, Zanzibar
imeanzisha rasmi Wakala wa Uchapaji wa Serikali Zanzibar, chini ya Wizara ya
Habari, Utalii na Mambo ya Kale ambapo Wakala hiyo imepewa uwezo kisheria wa
kutoa huduma za uchapaji. Kwa upande wa Tanzania Bara, Idara ya Mpiga chapa
Mkuu wa serikali ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwa na jukumu la kutoa huduma ya uchapaji.
Idara ya Mpiga Chapa Mkuu
wa serikali imeabainisha lengo lake kuu kuwa,
ni Kutoa huduma za Uchapaji kwa wakati zenye ubora na kwa gharama nafuu. Idara hiyo inaongozwa
na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali ambaye
husimamia vitengo vya Udhibiti wa Ubora, Uzalishaji, Ufundi, Masoko na Maduka
ya Vitabu ya Serikali.
MWISHO
P1
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Uchapaji wa Serikali Zanzibar, Khalfan Sheikh Saleh, wakati
akimueleza namna Wakala unavyotekeleza majukuu yake wakati alipotembelea Wakala
huo, Maruhubi, Zanzibar.
P2
Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko akisisitiza umuhimu
wa mashine za kidigitali wakati alipotembelea Wakala wa Uchapaji wa Serikali
Zanzibar, , wakati alipotembelea Wakala huo, Maruhubi, Zanzibar.
P3
Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko akiangalia namna
mashine za kidigitali zinavyofanya kazi ya uchapaji wakati alipotembelea Wakala
wa Uchapaji wa Serikali Zanzibar, Maruhubi, Zanzibar.
P4
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko akiongea na baadhi ya
wafanyakazi wa Wakala wa Uchapaji wa Serikali Zanzibar, , wakati alipotembelea
Wakala huo, Maruhubi, Zanzibar.
P5
Mmoja wa Watumishi wa Wakala wa Uchapaji wa Serikali Zanzibar, akiendelea
na shughuli za Uchapaji kwa kutumia mashine ya Kidigitali kwenye kiwanda cha
Wakala huo.
No comments:
Post a Comment