Mtaalam wa Huduma za Kidijitali kutoka Tigo, Ikunda Ngowi,akimkabidhi mfano wa hundi ya 13m/- mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha Bongo 2020 Miller Said Kungwi, mkaazi wa Mbagala, Dar es Salaam.
WATEJA 1,904 wa Kampuni
ya Tigo Tanzania wamejinyakulia shilingi milioni 197.5 kupitia promosheni ya
Chemsha Bongo.
Hayo yalisemwa na Mtaalam
wa Huduma za Kidijitali wa Tigo, Ikunda Ngowi, wakati akimkabidhi mfano wa
hundi mshindi wa jumla ya promosheni hiyo Miller Kungwi kutoka Mbagala jijini
Dar es Salaam, aliyeibuka mshindi wa jumla na kupata shilingi milioni 13.
Alisema promosheni hiyo
ilianza Oktoba 2018 ambapo Watanzania 1,904 wameshiriki na Kungwi ameibuka
mshindi wa jumla hivyo kuwaomba Watanzania kuendelea kushiriki katika awamu ya
sita ya promosheni hiyo.
Ngowi alimpongeza
mshindi huyo kwa kutumia fursa hiyo na kuwashukuru wateja wote wa Tigo ambao
walishiriki na baadhi yao kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi za fedha
taslimu ambazo zinatolewa na kampuni hiyo.
“Tunayo furaha kubwa
kumkabidhi mshindi wetu fedha zake. Tunawashukuru wateja wetu nchi nzima
walioshiriki kwenye promosheni hii ya miezi mitatu ambayo sasa imemalizika”.
alisema Ikunda.
Mtaalam huyo alisema
pamoja na fedha pia kupitia promosheni hiyo wametoa simu 30 na gari moja aina
ya Renault Kwid lenye thamani ya shilingi milioni 23.
Alisema Tigo imeamua
kurejesha fadhila kwa wateja wake na kuahidi kuwa wataendelea kuboresha huduma
zao ili wateja wao waweze kufurahi.
“Mwisho wa promosheni
hii ni mwanzo wa nyingine hivyo tunawaomba wateja wetu kuendelea kucheza ili
waweze kujinyakulia zawadi,” alisema.
Kwa upande wake Kungwi alishukuru
kuibuka mshindi na kuahidi kuzitumia katika kufanikisha maendeleo ya familia
yake.
Kungwi alisema “Wakati
napigiwa simu, nilikuwa nyumbani najipanga kutoka kwenda katika mihangaiko
yangu ya kibiashara, nilipopata ile taarifa kwamba nimeibuka mshindi nilifurahi
sana, kwani sikutegemea kabisa kuwa ningeibuka mshindi katika promosheni hii.
Habari hizi naziona
kama ndoto kwangu, nashukuru Tigo kwa kunipa zawadi hii kwani itanisaidia
kujiajiri na kuisaidia familia yangu “alisema.
No comments:
Post a Comment