Kufuatia Kaya 250 katika kata ya Msolwa Stesheni katika kijiji cha
Nyange Wilayani Kilombero kuathirika na athari za maafa ya mafuriko. Kamati ya Usimamizi wa Maafa ya
Wilaya hiyo imeelekezwa kufanya tathmini ya awali kwa kata ya Mbanane na
Kichangani ambazo takribani watu 350 wameathiriika na maafa hayo
yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini.
Akiongea mara baada ya kukagua athari za maafa katika kata hizo,
wilayani Kilombero, Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya maafa Ofisi ya Waziri
Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, amesema tathmini ya awali ya athari za maafa katika
kata hizo hainabudi kufanyika kwa haraka ili kubaini hatua za kuchukua katika
kukabiliana na maafa hayo.
“Kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa maafa
Na. 7 ya mwaka 2015, inaainisha majukumu ya kamati za usimamizi wa
Maafa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi mkoa, ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo,
jukumu la msingi ni kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika
ngazi husika, pamoja na Kuratibu na kusimamia shughuli za usimamizi wa
maafa na operesheni za dharura ndani ya Kijiji wilaya au mkoa. Hivyo
kamati hii haina budi kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.”amesisitiza Kanali Matamwe
Awali akieeleza hatua ambazo
kamati ya Menejimenti Usimamizi wa Maafa ya Wilaya hiyo ilizo zichukua, Mkuu wa
Wilaya ya Kilombero, Mhe. James Ihunyo, amefafanua kuwa hadi kufikia tarehe 20
Machi 2020, kamati hiyo ilikuwa imefanikiwa kuwaokoa watu 350 ambao wamehifadhiwa
kwenye shule ya sekondari Nyange.
“Tunaishukuru serikali
kupitia, Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya uratibu wa shughuli za maafa kwa miongozo, lakini pia na kufika kwa wakati
katika kata zetu, tumefurahi na mmetuletea mablanketi ambayo naamini yatawasaidia
waathirika wa maafa haya ambao tumewahifadhi hapa shuleni. Kwa sasa wapo
wanaume 172 na wanawake 178 huku watoto ni 30 ambao tumewahifadhi” Ameeleza Mhe. Ihunyo.
Kwa mujibu wa Taarifa ya
Mamlaka ya Hali hewa iliyotolewa mwezi Februari mwaka huu imeeleza kuwa
kutakuwa na mvua za juu ya wastani katika eneo kubwa la nchi kati ya mwezi
Machi hadi mwezi Mei, mwak huu, ambapo mvu ahizo zilitarajiwa kuanza kati ya
wiki ya kwanza au ya pili ya mwezi Machi na kutaraji akumaliziaka kati ya wiki
ya kwanza au ya pili yamwezi Mei. Hivyo kutokana na mvua hizo wananchi
hawanbudi kuchukua tahadhari za athari za mvua hizo.
No comments:
Post a Comment