Naibu
Waziri ,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akikagua nyumba zilizojengwa na Watumishi Housing Company eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company Dkt. Fred Msemwa.
Mkurugenzi wa Watumishi Housing Company, Dkt. Fred Msemwa akitoa maelezo kuhusu
mradi wa nyumba za kampuni hiyo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi ujenzi wa
nyumba eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Dkt. Mary akitoa ushauri juu ya upangishaji na uuzaji wa nyumba kwa
watendaji wa Watumishi Housing Company katika mojawapo ya nyumba
alizozikagua eneo la Gezaulole - Kigamboni jijini Dar Es salaam.
Baadhi ya Nyumba za ghorofa za Mradi wa Watumishi Housing Company zilizojengwa
kwa madhumuni ya kuuziwa Watumishi wa Umma na kupangishwa katika eneo
la Gezaulole Kigamboni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Na Aaron Mrikaria - Dar es Salaam
Menejimenti ya Watumishi Housing Company
yashauriwa kutenga baadhi ya nyumba zilizojengwa na kampuni hiyo kwa
ajili ya kuwapangisha Wadau wa Mifuko ya Jamii ili nao wanufaike na Mradi huo
wa Nyumba za bei nafuu.
Ushauri huo umetolewa naNaibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ta Utumishi wa umma na Utawala Bora, Dkt.
Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa ziara yake ya kikazi leo alipotembelea mradi wa
nyumba wa kampuni hiyo katika eneo la
Gezaulole Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar
es Salaam.
“Kutokana
na uhalisia kwamba fedha za ujenzi wa Mradi wa Nyumba hizi unatokana pia na
mchango wa fedha za wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, ni vema nao
wakanufaika kwa kuuziwa baadhi ya nyumba hizi, kwa maana hiyo tutakuwa
tumetenda haki kwa Watumishi wa Umma lakini pia tutakuwa tumetenda haki kwa
wadau wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.’’
Aidha, Dkt. Mwanjelwa ameitaka
Menejimenti ya Watumishi Housing Company kumchukulia hatua za
kisheria mkandarasi anayejenga tangi la maji katika mradi huo (CRJE) kutoka
nchini China, endapo atashindwa kumaliza kazi hiyo kwa wakati.
Pia, Dkt. Mwanjelwa ameiagiza
kampuni hiyo kuanza kumkata mkandarasi Hugo fedha za malipo ya kazi hiyo kwa
mujibu wa makubaliano ya mkataba kama njia mojawapo ya kutoa fundisho kwa
wakandarasi wanaozembea kumaliza ujenzi wa miradi kwa wakati.
Sanjari na hayo, Dkt.
Mwanjelwa ameipongeza Watumishi Housing
Company kwa ubunifu wa kujenga
nyumba za gharama nafuu, na kati ikiwa ni pamoja na kutoa fursa kwa wananchi
kupanga katika nyumba hizo.
No comments:
Post a Comment