HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 05, 2020

MENEJA WA TANROAD MORO AREJESHWE WIZARANI-MAJALIWA

*Ni baada ya kushindwa kukagua madaraja kwenye eneo lake 
 Eneo la daraja la Kiyegeya  ambalo lilisombwa na maji na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara kati ya Morogoro na Dodoma , ukarabati wake unaendelea.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya ukarabati wa daraja la Kiyegeya lililopo eneo la Gairo  ambalo llimesombwa na maji  na kusababisha kukatika kwa mawasiliano  ya barabara ya barabara kati ya Morogoro na Dodoma, Machi 4, 2020. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya ukarabati wa daraja la Kiyegeya  lililopo  eno la Gairo ambalo limesombwa na maji   na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara kati ya Morogoro na Dar es salaam, Machi 4, 2020. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Isack Kamwelwe. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipita kwenye msururu wa magari  yaliyokwama baada ya daraja la Kiyegeya kusombwa  na maji na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara  kati ya Morogoro na Dodoma, Machi 4, 2020.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa pole baadhi ya madreva na abiria waliokwama baada ya daraja la Kiyegeya  kusombwa na maji na kusababisha  kukatika  kwa  mawasiliano ya barabara kati ya Morogoro na Dodoma, Machi 4, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Na Mwandishi Maalum

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD), mkoa wa Morogoro, Mhandisi Godwin Andalwisye arejeshwe wizarani na nafasi yake ijazwe na mtu mwingine mara moja baada ya kuzembea kutimiza wajibu wake.
Pia, Waziri Mkuu ametoa onyo kwa Mameneja wa TANROAD wa mikoa yote nchini waache kukaa maofisini na badala yake wahakikishe wanatekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa madaraja yote ili kujiridhisha na hali ya usalama hususani katika kipindi hiki cha mvua.
Uamuzi huo umekuja baada ya kiongozi huyo kushindwa kufanya ukaguzi wa usala wa madaraja yaliyoko kwenye mkoa wake na kubaini kama kuna daraja linamatatizo hali iliyosababisha daraja la Kiyegeya lililopo wilayani Kilosa ambalo linaunganisha mkoa wa Morogoro na Dodoma kuvunjika.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo(Jumatano, Machi 4, 2020) baada ya kutembelea eneo hilo na kukagua ukarabati ili kurejesha mawasiliano ya barabara. Waziri Mkuu ameshuhudia mrundikano wa magari na abiria hali ambayo haikumfurahisha.
“Hivi unajua udhahifu wako ni kwa sababu hukufanya ukaguzi kuona kama daraja limejaa mchanga au uchafu ambao umesababisha kipenyo cha kupitisha maji kuwa kidogo na maji yakalazimika kupanda juu hali ambayo ilisababisha daraja hili kusombwa na maji.”
Amesema wakati njia hiyo inarekebishwa itengenezwe njia nyingine ya muda ili kuweza kupitisha magari na kisha Serikali itachukua hatua baada ya kubaini nini kimesababisha.  
Ili kuharakisha kazi hiyo inakamilika kwa haraka, Waziri Mkuu ameagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwelwe, Katibu Mkuu wa wizara hiyo pamoja na wahandisi wote wa TANROAD mkoa wa Morogoro na Dodoma leo wakutane kwenye eneo la tukio na wahakikishe kuanzia kesho (Alhamisi, Machi 5, 2020) njia hiyo iwe imefunguka.
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema atawasiliana na Mkuu wa Majeshi, Generali Venance Mabeyo ili aweze kupata msaada wa wanajeshi ili waongeze nguvu katika kuhakikisha kwamba mawasialaino yanarejea kwa haraka.
Akiwapa pole madereva na watumiaji wengine wa barabara waliokwama katika eneo hilo, Waziri Mkuu amesema “Nimetumwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuja kuwapa pole na kuwahakikisha kwamba Serikali inafanya kila linalowezekana ili kuifungua barabara hii.”

No comments:

Post a Comment

Pages