HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 05, 2020

Umeme wa chini ya ardhi wapigiwa debe

Na Happiness Mnale, Njombe

MFUMO wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines)umetajwa kuwa bora,salama na unaotunza mazingira tofauti na unaosafirishwa kwa kutandaza nguzo na nyaya.

Kauli hiyo imetolewa juzi katika ziara iliyofanyika Kijiji cha Matembwe, Wilaya ya Njombe ikiwa ni mpango wa mafunzo kwa wanahabari wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET)kuhusu nishati jadidifu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Cefa ambao ni wazalishaji wa umeme unaotumia maji, Johannes Kamonga, alisema kwamba umeme wao unasambazwa kwa kupitishwa ardhini kwani ni salama na nyaya zinadumu kwa muda mrefu.

“Mradi huu wa umeme unatekelezwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya CEFA iliyo chini ya Italia, tunasambaza katika vijiji nane vilivyo ndani ya kata za Ikondo,Matembwe na Lupembe na ziada inayobaki inaingizwa kwenye gridi ya Taifa,”alisema Kamonga.

Kamonga alisema kwamba wao ni wazalishaji wa mradi mdogo wa umeme(Mini grid) unaotokana na maporomoko ya maji katika Kata ya Ikondo ambapo hadi sasa wamesambaza katika kaya 911.

“Huu umeme tunaopitisha ardhini ni salama na unatunza mazingira na kuleta picha nzuri ya mji,”alisema.
Alisema umeme huo una nyaya zenye chuma maalum ya kuzuia ajali.

“Umeme wa ardhini ni salama, ni vyema taifa likaanza kutumia aina hii ya usafirishaji wa umeme, kwanza miji itapendeza hakutakuwa na nguzo na nyaya kila kona, lakini pia hazipigwi na radi,”alisema.

Akizungumzia changamoto wanazokutana nazo alisema ni nyaya za usambazaji kuwa gharama ya juu.

Kamonga alisema kwasasa wanatarajia kutanua huduma ili kuwafikia wanakijiji wa Kitoleambao hawana umeme.
Meneja mradi wa CEFA, Fabrizio Colombelli, alisema taasisi hiyo ipo nchini tangu mwaka 1976 na imejikita katika miradi ya umeme vijijini.

Alisema mradi wa umeme Matembwe umejengwa na CEFA na kusimamiwa na Kampuni ya kijiji cha Matembwe (MVP)ambapo unazalisha kilowati 430.
Alisema hadi sasa wana miaka zaidi ya 35 na hakuna madhara yoyote yamewahi kutokea tangu usambazaji wa umeme ulipoanza.

No comments:

Post a Comment

Pages