NA TIGANYA VINCENT
MRAJISI Msaidizi wa
Ushirika Mkoa wa Tabora ameagiza
kupeleka na kutaja majina ya watumishi na viongozi wanajihusisha na biashara haramu ya
mazao ya biashara ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Agizo hilo lilitolewa na
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa Kikao cha Ushauri cha
Mkoa(RCC) wa Tabora cha kupitia
mapendekezo ya bajeti ya 2020/21.
Alisema vitendo hivyo
vinawadhofisha wakulima na kuwafanya kuendelea kuwa masikini na Halmashauri za
Wilaya zinazolima mazao hao kupata mapato kidogo yanatoka na ushuru wa mazao.
Mwanri alisema haiwezekani kila wakati Ofisi ya Mrajisi Msaidizi inatoa
taarifa kuwa kuna baadhi ya viongozi wa serikali, wa siasa na Vyama vya Ushirika wamejiingiza kwenye biashara ya vishada na
uuzaji wa pembejeo bila kuwataja majina.
Alisema kuwa
Serikali kupitia Waziri Mkuu inashatoa maelekezo kuwa mtu akayeruhusiwa kuuza
tumbaku ni yule ambaye ana shamba la tumbaku na zao hilo litauzwa kupitia
ushirika.
Aidha Kamati hiyo
ya ushauri ya Mkoa wa Tabora imeviomba Vyombo vya Usalama ikiwemo Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza kuwafuatilia wanajihusiha
na vitendo hivyo ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Ilisema vitendo
hivyo ni kosa ikiwemo la rushwa na udanganyifu kwa ajili ya kumnyonya mkulima
na kuibia Serikali mapato yake yanatokana na ushuru wa mazao.
Katibu Tawala Mkoa
wa Tabora Msalika Makungu alisema kuna baadhi ya viongozi wanashiriki katika
biashara chafu ya uuzaji na ukopeshaji wa wakulima fedha kwa riba kubwa na
kuwafanya kuendelea kuwa masikini.
Alisema kuna baadhi
ya wakulima wamekuwa wakikopesha pembejeo na fedha kwa mara mbili ya bei halali
kwa madai kuwa pindi atakapovuna tumbaku ni lazima ampe sehemu ya tumbaku kama
malipo ya deni.
Makungu alisema
vitendo hivyo vimefanya wakulima wengi wakati wa kuuza tumbaku yao kubaki na
fedha kidogo ikiwa sehemu kubwa inaenda katika deni.
No comments:
Post a Comment