Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, akimsisitiza msanii wa bongofleva Rashid Abdallah maarufu kama Chid benz kufanya kazi kwa bidii na kuwa mbunifu huku akimhakikishia kuwa serikali ipo tayari kumpa ushirikiano alipokuwa akifanya kikao nae jijini Dodoma. (Picha na WHUSM).
Na Anitha Jonas – WHUSM
Naibu Waziri Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amwaahidi ushirikiano
msanii wa bongofleva nchini Rashid Abdallah maarufu Chidbenz.
Mheshimiwa Shonza ametoa kauli
hiyo leo jijini Dodoma alipofanya kikao na msanii huyo ambapo Chid benz
alimuhakikishia kuwa kwa sasa
amebadilika na anataka kuwaonyesha watanzania amefanikiwa kujikwamua
katika matumizi ya madawa ya kulevya na hataki tena kurudi huko kwani anazaidi
ya miezi mitatu sasa hajatumia madawa hayo kabisa.
“Kati ya wasanii wenye
kukubalika na mashabiki zao wewe Chid benz ni mmoja wao na mashabiki zako ni wengi hivyo
ningependa kukuona kwanzia sasa unalijenga zaidi jina lako kwa kuonyesha kuwa
umebadilika,katika kipindi hichi nitafurahi zaidi kukuona unasonga mbele na
hurudi tena katika matumizi ya madawa ya kulevya wizara ipo pamoja na wewe kukusaidia wakati wowote ,”alisema
Mhe.Shonza.
Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho mheshimiwa Shonza alimsisitiza
msanii huyo kuwaonyesha watanzania kuwa
anaweza na hata akipewa nafasi anaweza kujitumia vyema na kuonyesha juhudi yake katika kufanya kazi
na kuwa mbunifu katika kufanya kazi zake za usanii.
Naye Msanii huyo wa Bongofleva
Chid benz alieleza kuwa kwa sasa hautarudi nyuma tena sababu tayari amekwisha
acha kutumia matumizi ya madawa hayo na
ninaelewa bahati haiji mara mbili lakini kwangu naiona imekuja zaidi ya mara
moja kwa maana ya kuwa nimekuwa nimekuwa na anguka nainuka narudi kwa mashabiki
wananipokea nakuendelea kukubali muziki wangu hakika najiona niwakati wa
kuwafurahisha zaidi mashabiki na sitawaangusha.
“Ombi langu kwa serikali ni kupata
ushirikiano na mapema wiki ijayo ninatarajia kutoa wimbo wangu mmoja uitwao Beautiful
ambao nimeuiamba nikisifu uzuri wa mwanamke na kufuatia janga la Corona
ninamwahidi mheshimiwa Naibu Waziri kuwa nitatunga wimbo kwa ajili ya Corona ,”Chid
benz.
Pamoja na hayo nae Chid benz
alitoa wito kwa watanzania kuacha kufanya mzaha katika mitandao ya jamii kuhusu
suala la ugongwa Corona sababu hili ni tatizo ni janga linalosumbua dunia kwa
sasa hivyo jambo la msingi ni kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na serikali
kutoka kwa wataalamu wa afya.
No comments:
Post a Comment