Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Tawi la Mawasiliano wakati akifungua kikao cha Baraza hilo, Dodoma.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto) akiwasili ukumbini kufungua Baraza la Wafanyakazi wa Tawi la Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano lililofanyika Dodoma. Kulia ni Kitolina Kippa, Kaimu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano wa wizara hiyo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Kitolina Kippa akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye kufungua Baraza la Wafanyakazi wa Sekta hiyo, Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Tawi la Mawasiliano wakiimba wimbo wa wafanyakazi wa mshikamano daima “solidarity forever” wakati wa kikao cha Baraza hilo kilichofanyika Dodoma.
Mwenyekiti wa wanawake wa TUGHE, Tawi la Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Grace Chalila akitoa salamu za shukrani kwa Mgeni Rasmi,
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye baada ya kufungua Baraza hilo lililofanyika Dodoma.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye baada ya kufungua Baraza hilo lililofanyika Dodoma.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyevaa tai aliyesimama mstari wa mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Tawi la Mawasiliano, Sekta ya Mawasiliano.
Na Mwandishi Wetu
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi
Atashasta Nditiye amesema kuwa Sekta ya Mawasiliano ni sekta mtambuka ambayo ina mchango mkubwa katika kuinua pato la Taifa hivyo ni budi
watendaji wake kufanya kazi kwa bidii,
ufanisi na kutoa huduma bora kwa jamii
ili iwe ya kwanza katika kuchangia pato la taifa.
Mhandisi Nditiye
ameyasema hayo alipokuwa anafungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya
Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano uliofanyika katika
ukumbi wa Kituo Cha Mikutano Cha Dodoma mkoani Dodoma.
“Sekta ya
Mawasiliano ni sekta ambayo taasisi za Serikali, sekta ya umma na binafsi
zinategemea huduma za mawasiliano, sisi ndio wasimamizi na watunga sera ambapo
tunahitajika kuhakikisha mawasiliano yanajitosheleza kwenye dunia ya kisasa
ambayo inapelekea dunia kuwa kijiji kimoja”, amesema Mhandisi Nditiye.
Aidha, amesisitiza
kuwa Sekta ya Mawasiliano ina uwezo wa kufanya vizuri zaidi katika kuchangia
pato la taifa kwa kuwatumia vema wataalamu wa Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) wenye weledi na wabunifu ili waweze kuisaidia Serikali katika
jukumu zima la kuwahudumia wananchi kwa kuwa Sekta hii imekuwa inaongoza kwa
kuchangia pato la taifa katika kipindi cha mwaka 2017/2018 kwa kushika nafasi
ya tatu ambapo imechangia asilimia 13.4 ya pato la taifa na imeendelea kuongoza
na kuwa kati ya tano bora ya vyanzo vikuu vya mapato nchini.
Akizungumzia
umuhimu wa Baraza la Wafanyakazi, alisema kuwa Baraza ni kiungo muhimu
kuwezesha Menejimenti kutimiza majukumu yake na kusimamia mwenendo mzima wa
utendaji kazi wa Wizara na Sekta kwa ujumla kwa mujibu wa majukumu yake hivyo
ni vema kuhakikisha kuwa viongozi na watumishi wanashirikiana katika kutekeleza
majukumu yao kwa kuwa kila mmoja anategemea uwepo wa mwingine
Naye Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano),
Kitolina Kippa amesema kuwa katika kikao
hicho, wajumbe watapokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Sekta kwa
kipindi cha mwaka wa fedha wa 2019/2020 ikiwa ni pamoja na ujenzi wa
miundombinu ya TEHAMA na utoaji wa huduma za mawasiliano ndani ya Serikali na
kwa wananchi ili kuhakikisha kuwa huduma zinapatikana kwa wakati na kwa
uhakika; kupitia mipango iliyoandaliwa kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji wa
majukumu ya Sekta kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021 pamoja na kutoa mafunzo ya
kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu janga la UKIMWI, maambukizi ya magonjwa
yatokanayo na lishe; na kuwataka watumishi wa umma kushirikiana kwa pamoja na
kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa
umma ili Serikali iweze kuwahudumia wananchi wake ipasavyo
Naye
Mwenyekiti wa Wanawake wa Tawi la Mawasiliano, Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Grace Chalila ameuomba uongozi wa Wizara
kuiomba Serikali iongeze bajeti ya Sekta ya Mawasiliano ili iweze kuchangia
zaidi pato la taifa tofauti na inavyochangia sasa kwa kuwa watalaamu wapo na
wanaweza kutoa huduma za mawasiliano kwa wananchi na Serikali yenyewe kwa
kuzingatia kuwa Serikali inatumia na kutegemea kwa kiasi kikubwa matumizi ya
TEHAMA na mifumo ya kielektroniki na huduma mtandao ikiwemo Serikali mtandao,
elimu mtandao, afya mtandao na ukusanyaji wa kodi na mapato ya Serikali
Katika
hatua nyingine, Mhandisi Nditiye amewakumbusha wafanyakazi kuwa ugonjwa wa
UKIMWI upo na amewataka wajilinde na kujali afya zao kwa kuwa Serikali
inawategemea katika kutekeleza majukumu yao ili waweze kuwahudumia wananchi
Vile vile,
amewataka wazingatie maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya nchini kwa
kuzingatia usafi na kuepuka kusalimiana kwa kutumia mikono na wanawe mikono
kila wakati kwa kuwa virusi vya Corona vimeingia nchini na tayari imeripotiwa
kuwa mwananchi mmoja amebainika kuwa na COVID 19
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment