Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akifungua jana kongamano la siku mbili
la vijana katika fursa za kilimo , mifugo na uvuvi ambao wameoka Tabora, Kigoma na Singida.
NA TIGANYA VINCENT
VIJANA wametakiwa kutumia fursa zinazotokana
shughuli za kilimo na ufugaji kujiari wenyewe badala ya kusubiri ajira za
Serikali ili wawaze kujiongezea kipato kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe na
Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa
wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifungua kongamano la vijana katika fursa za
kilimo , mifugo na uvuvi kwa washiriki
toka Tabora, Kigoma na Singida.
Alisema Serikali kupitia Wizara ya
Nishati, imejitahidi kufikisha umeme vijijini ambako ndiko mazao yanapatikana
ili kuweza kuyaongezea thamani kwa kuyasindika.
Mwanri alisema hiyo ni fursa nzuri kwa
vijana ya kutumia umeme ilikufanya kazi za kuzalisha na kuchakata mazao ya kilimo,
mifugo na uvuvi hivyo kuongeza thamani na uhakika wa soko na bei nzuri.
Alisema uzalishaji wa mbegu bora za mazao
nchini una uhitaji mkubwa na takwmi zinaonyesha kuwa mahitaji ya mbegu ni tani 187,000
kwa mwaka wakati uzalishaji wa ndani ni tani 71,000.
Mwanri aliongeza kuwa eneo hilo lina
fursa kubwa kwa vijana kuzalisha mbegu kwani zinzhitajika kwa wingi.
Alisema eneo jingine ambalo ni fursa kwa
vijana ni kilimo cha mazao ya mafuta ambapo mahitaji ya mafuta ya kula ni lita 650,000
kwa mwaka wakati uwezo wa nchi ni kuzalisha lita chini ya 250,000.
Mwanri alisema hali hiyo inatoa fursa
kubwa kwa vijana kuzalisha mazao ya alizeti na michikichi.
Kwa upande wa Mratibu wa Mkakati wa Taifa
wa Vijana kushiriki katika Kilimo Revelian Ngaiza alisema lengo kongamano hilo
ni kutoa elimu kwa vijana nchini ili waweze kushiriki katika uzalishaji mali
kupitia kilimo na ufugaji ili waweze kuinua kipato cha na Taifa kwa ujumla.
Alisema
kauli mbiu yetu ni “vijana,kilimo ni ajira” imelenga kuwasaidia vijana kutambua
na kufanya kilimo kuwa nguzo ya upatikanaji ajira nyingi zaidi.
No comments:
Post a Comment