HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 03, 2020

Vijana Wapo Hatarini Kupata Matatizo ya Usikivu

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo wa MNH-Mloganzila, Dk. Jonas Ndasika, akimfanyia uchunguzi wa awali mtoto Lailat Mohamed aliyefika hospitalini hapa kwa ajili ya kupimwa usikivu.


Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Idara ya Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dk. Edwin Liyombo amesema 1.1 bilioni ya vijana wenye umri kati ya miaka 12 hadi 35 wako katika hatari ya kupata matatizo ya usikivu kutokana na mtindo mbaya wa maisha kama vile kwenda mara kwa mara katika kumbi za starehe zenye kelele za muziki hasa disko.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Machi 3, mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya usikivu diniani yaliyofanyika katika Hospitali ya Muhimbili - Mlongabzila lengo ikiwa ni kuchunguza kiwango cha usikivu kwa wananchi.Dk. Liyombo anesema takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha takribani watu 466 milioni wana matatizo ya usikivu ambapo hadi kufikia 2050 idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka hadi kufikia milioni 900.

Ameesema  milioni 1.1 ya vijana wenye umri kati ya miaka 12 hadi 35 wako katika hatari kubwa ya kupata matatizo ya usikivu kutokana na mtindo mbaya wa maisha.

Dk. Liyombo ametaja sababu zingine zinazosababisha tatizo hilo kuwa ni pamoja na matumizi mabaya ya dawa bila kuzingatia ushauri wa daktari, magonjwa ya kurithi, maambukizi kwa mama wakati wa ujauzito na matatizo wakati wa kujifungua.


 “Ziko sababu nyingi zinazosababisha matatizo ya usikivu kwa watu ikiwa ni pamoja na maambukizi kwa mama mjamzito wakati wa ujauzito unaoweza kupelekea matatizo kwa mtoto, magonjwa ya kurithi, matatizo wakati wa kujifungua pamoja na matumizi mabaya ya dawa bila kufuata masharti ya daktari lakini pia ziko dawa zinazochangia matatizo haya hivyo anayetoa dawa hizo inampasa kuwa na ujuzi wa kutosha kabla ya kumpatia mtumiaji” amefafanua Dk. Liyombo.

Aidha Dk. Liyombo ametoa wito kwa watanzania kujijengea utamaduni wa kupima usikivu kila mara ili kujikinga na madhara yanayoweza kuzuiliwa mapema kabla ya kupoteza usikivu.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo wa MNH-Mloganzila, Dk. Jaria Rahib ametaja idadi ya wagonjwa walioonwa na wataalam wakati zoezi hili lilipofanyika mwaka jana kwa muda wa siku 3 kuwa ni 497 ambapo kati yao 197 walikutwa na matatizo ya usikivu pamoja na magonjwa mengine ya masikio yaliyohitaji matibabu lakini kwa leo tumewaona wagonjwa takribani 150.

“Mwaka jana tulipofanya zoezi hili kwa muda wa siku 3 tuliwaona wagonjwa 497 kati yao 197 walikutwa na matatizo ya usikivu pamoja na magonjwa mengine ya masikio yaliyohitaji tiba lakini kwa leo tumefanikiwa kuwaona wagonjwa wapatao 150” ameeleza Dk. Rahib.

Zoezi la kupima kiwango cha usikivu, kutoa elimu na ushauri limefanyika bila malipo ambapo wananchi waliobainika kuwa na matatizo mbalimbali wamepatiwa rufaa ya kuendelea na matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kufuata utaratibu wa kawaida wa hospitali.

Katika maadhimisho hayo
Wananchi wajitokeza kupimwa usikivu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila katika kuadhimisha siku ya usikivu duniani yenye

Kauli mbiuya maadhimisho hayo ni “Usiruhusu upotevu wa usikivu uwe kikwazo, usikivu bora kwa maisha bora”

No comments:

Post a Comment

Pages