Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza katika kikao kazi cha
Mawaziri na Makatibu Wakuu cha kujadili virusi vya Corona (COVID- 19)
nchini kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Machi 23, 2020. Katikati
ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Zainab Chaula. (Picha na OIfisi ya Waziri
Mkuu).
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea kufanya tathmini ili
kuhakikisha inazuia ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na
virusi vya corona (COVID-19) isiweze kusambaa kwa kiasi kikubwa nchini.
Pia,
Waziri Mkuu amevishukuru vyombo vya habari nchini kwa ushirikiano
wanaoutoa kwa Serikali katika kuelimisha umma namna ya kujikinga na
virusi vya corona.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Machi 23, 2020) wakati
akizungumza na Mawaziri na Makati Wakuu katika Kikao Kazi kilichofanyika
kwenye ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma.
Imeelezwa
kuwa kinga dhidi ya virusi vya corona liwe ni jambo la kimkakati zaidi
kuliko kusubiri kutibu, hivyo kwa sasa Serikali imeweka mkazo kwenye
kuwahamasisha wananchi kujikinga na virusi hivyo.
“…Mawaziri
hakikisheni katika kipindi hiki ziara za kwenda kukagua miradi
zielekezwe kwa Wakurugenzi ikibidi kwa Makatibu Wakuu, Mawaziri
mnatakiwa mjikite katika kukinga Taifa na corona.”
Wakati huo huo,
Waziri Mkuu amesema Serikali imeunda kamati tatu kwa ajili ya
kukabiliana na homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi ya corona
(COVID-19). Kamati hizo ni ya Kitaifa ambayo itaongozwa na Waziri Mkuu
na itahusisha baadhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu na Msemaji Mkuu wa
Serikali.
Kamati
ya pili ni ya Makatibu Wakuu kutoka sekta husika na itaongozwa na
Katibu Mkuu Kiongozi na kamati ya tatu ni ya Kikosi Kazi cha Taifa
ambacho kitaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto huku wajumbe wake wakiwa ni wataalamu
akiwemo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Awali,Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
alisema katika kipindi cha saa 24 jumla ya watu 292,142 duniani
walibainika kuwa na virusi vya corona kati yao watu 12,784 walifariki.
Pia,
katika Bara la Afrika watu 736 walibainika kuwa na virusi vya corona na
kati yake watu 20 walifariki katika kipindi cha saa 24.
Akizungumzia
kwa upande wa Tanzania, Waziri Ummy alisema jumla ya watu 12
walibainika kuwa na virusi vya corona tangu mgonjwa wa kwanza
alivyogundulika nchini na kwamba wagonjwa wote hali zao ni nzuri na
mmoja amepimwa zaidi ya mara mbili na kubainika kuwa hana virusi.
No comments:
Post a Comment