Dar es Salaam 06 April 2020 - Benki ya Stanbic
Tanzania imemteua Kevin Wingfield kuwa Mkurugenzi Mkuu kuanzia tarehe 01 Aprili
2020.
Wingfield anachukua nafasi ya Ken Cockerill
ambae ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Standard Bank nchini Lesotho.
Safari ya Wingfield ilianza mwaka 1998, katika
taasisi ya Standard Bank Group, mpaka sasa ana uzoefu wa zaidi miaka ishirini.
Wingfield ameshika nyadhifa mbalimbali ndani ya taasisi hiyo ikiwemo;
Mkurugenzi wa maendeleo ya kimkakati kwa wateja, huduma za kibenki za watu
binafsi na biashara - Standard Bank Africa; Mkurugenzi wa huduma za kibenki za
watu binafsi na biashara - Standard Bank Ghana; na Mkurugenzi wa huduma za
kibenki za watu binafsi na biashara - Stanbic Bank Uganda.
Katika wadhifa wake huu mpya, Wingfield
anategemewa kuongoza ukuaji wa benki, na kuendeleza ubunifu na uvumbuzi ambao utawezesha
mafanikio ya kifedha ya watu na biashara nchini Tanzania. Pia kuunga mkono
mpango wa kukuza uchumi kupitia uwekezaji katika viwanda na uboreshaji wa
miundombinu.
Akizungumza juu ya uteuzi huo, Mwenyekiti wa
Bodi ya Benki ya Stanbic Tanzania, Mark Mwandosya alisema, “Wingfield anawito
wa uongozi, taaluma na uzoefu ambao ameupata kwa kufanya kazi katika masoko
mbalimbali barani Afrika. Tunaimani kwamba chini ya uongozi wake, benki hii
itaendelea kukua na kuchangia maendeleo ya nchi yetu.”
No comments:
Post a Comment