Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, George Simbachawene, akizungumza na Uongozi wa Jeshi la Polisi
Wilayani Mpwapwa wakati wa ziara ya kikazi wilayani hapo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Mkuu wa Polisi Wilaya ya
Mpwapwa, Mrakibu wa Polisi, Cosmas Mboya, akitoa Taarifa ya Ulinzi na Usalama
kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene wakati wa ziara ya
kikazi wilayani hapo.
Na Mwandishi Wetu, Mpwapwa
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameupongeza uongozi wa Jeshi la Polisi
wilayani Mpwapwa kwa kudhibiti matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo wizi wa
mifugo, mauaji, ubakaji, wizi wa pikipiki, uchomaji moto nyumba, dawa za
kulevya, kuzini na maharimu na kupoatikana na silaha kinyume cha sheria.
Waziri Simbachawene
ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika wilaya hiyo ambapo alipokea Taarifa
ya Polisi ya wilaya hiyo yenye jumla ya wakazi 303,202 wakiwemo wanaume 153,415
na wanawake 158,331 kwa mujibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka 2012 huku
mpaka sasa ongezeko la watu ni asilimia 2.1. %
“Nakupongeza OCD Mboya
na askari wote walioko chini yako kwa jinsi mnavyoendelea kuimarisha ulinzi na
usalama katika wilaya hii,muendelee na moyo huo huo na sisi kama serikali
tutaendelea kuwapa na kuwaongezea nguvu ili muweze kufanya kazi hii ngumu ya
kuzuia uhalifu na kuwalinda wananchi ili waweze kufanya shughuli za maendeleo
kwa amani na salama” alisema Simbachawene
Awali akisoma takwimu
za uhalifu mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene,Mkuu
wa Polisi Wilaya ya Mpwapwa,Mrakibu wa Polisi, Cosmas Mboya aliweka wazi
kupungua kwa makosa mbalimbali ikiwemo wizi wa pikipiki kutoka pikipiki 27
mwaka 2018 hadi pikipiki 7 mwaka 2019, wizi wa njia ya mtandao matukio 28 mpaka
17,kuchoma moto nyumba matukio 7 mpaka 2,dawa za kulevya tukio 1 huku hakuna
tukio lilitokea mwaka 2019,ulimaji wa bangi tukio 1 huku hakuna tukio
lililoripotiwa mwaka 2019.
Aidha akielezea suala
la matukio ya usawa wa kijinsia Mrakibu wa Polisi,Cosmas Mboya alisema kumekuwa
na upungufu wa matukio hayo yamepungua kutokana na kuwepo kwa dawati la jinsia
wilayani hapo.
“Dawati la Jinsia na
watoto limeendelea kufanya kazi kwa kushauri na kusimamia kesi zinazohusu
unyanyasaji wa kijinsia na watoto,huku likiwa msaada mkubwa kwa wakazi ikiwemo
wanaume wanaonyanyaswa na wake zao kufika kwenye dawati hilo na kuleta
malalamiko huku jumla ya kesi hizo kwa mwaka 2018 ni 874 zikishuka mpaka 718
kwa mwaka 2019” alisema Mboya.
No comments:
Post a Comment